Kama kuna kitu kizuri ambacho kimetokana na maswala ya globalization, basi ni uwezo wa mtu yeyote yule kuigeuza mitandao kua fursa ya kujiajiri na kuanza kujiingizia kipato. Iwe ni Part-Time au Full Time.
Mitandao ikitumika vizuri na kwa usahihi, basi inaweza fanikisha yote haya.Jambo la kutilia maanani mapema kabisa ni kuelewa kwamba hakunaga pesa za bure bure. Hakuna pesa utapata kwa kufuata shortcut. Hakuna pesa za kudownload.
Hivyo kama hiki ni kitu ambacho uko interested nacho, kua tayari kukipa u serious ambao ungeweka let’s say ungekua unafungua biashara phyisical (brick and mortar business) kama duka, nk.
Hakikisha kua uko tayari kuwekeza muda, ujuzi wako na inapobidi; pesa.Kwenye makala hii nita focus sana na swala la kujiajiri online, kwa kuanzisha biashara yako mwenyewe.
Pia Soma: Kuingiza Pesa Mtandaoni: Yote Unayobidi Kufahamu
Background Kidogo

Hizi mambo za mitandao, financial independence na kujiajiri zimeanza kuni- interest miaka kadhaa nyuma. Kuingiza pesa mtandaoni ilikua ni kitu nilichokua najua kinawezekana, lakini sikua najua inawezekana vipi. But I was willing to learn.
Namna yeyote ile niliyokuwa nakutana nayo online iki promise kukuingizia hela, jua nimeijaribu. Na kwa kua nlikua najaribu kila kitu nlichokua nikikutana nacho, basi naweza sema kuna baadhi ya mambo yamenipotezea muda na hayajaniletea matokeo yeyote yale.
Nimefanya hizo mambo za PPC (Getting Paid Per Click), PPV ( Getting Paid Per View/Kulipwa Kuangalia Matangazo/Video) na izo MicroTasks na utumbo mwingine. Hapa effort nliyokua naweka na hela niliyokuwa napata vilikua hata haviendani. Kuhangaika week nzima na mi vitu afu ikuingizie $1 ni utumbo kidogo.

Yapo mambo ambayo kwa kuyajaribu nimeishiwa kutapeliwa tena na tena. Nimejiunga na mi platform ya investments. Nime join masterclasses na ma course ya ma guru kibao walokua wananpromise kufika mwisho wa course zao nitakua na uwezo wa kuingiza pesa ndefu ila wapi. Nimejaribu mambo za kununua odds, fixed matches na utumbo mwingine tena na tena hadi akili iliponikaa sawa haha.
Kuna mambo ambayo yalikua promising lakini mwishowe hayakuleta faida yeyote. Lakini pia, yapo mambo ambayo nimeyakomalia na yakaniletea matokeo ambayo yanafaa kuitwa matokeo. Aina hii ya mambo ndio ninayo yaongelea kwenye Blog hii.
Pia Soma: Namna 37 Za Uhakika Unaweza Tumia Kujiingiza Pesa Mtandaoni
Now naweza sema to some extent, nimejiajiri kutumia hii hii mitandao in more than ten ways. Mambo sio mazuri saaana kivo, ila nimeona matokeo yale niliyokua nikiyatafuta and in some ways, zaidi hata ya yale niliyokua nayatafuta.
That said, kama unataka kuanza kuitumia mitandao kwa usahihi na ikibidi kujiajiri kabisa, basi zingatia yafuatayo;
1. Kua Na Ujuzi Unaolipa

Kama unaenda kuingiza pesa mtandaoni, basi inaenda kua either kwa kutumia ujuzi fulani ulionao kwenye mambo yako mwenyewe yatakayo kuingizia pesa au kuutumia ujuzi huo ulionao kukamilisha mambo ya watu wengine ambao in return watakulipa.
Yaani utaingiza pesa online kwa kuanzisha kitu ambacho utakua unafanya mwenyewe au kwa kuwafanyia wengine. Either way unahitaji ujuzi.Na sio ujuzi tu, bali ujuzi unaolipa. Swali la kujiuliza hapa ni ‘Una kitu gani ambacho unaweza kukifanya kutumia simu/tablet/laptop/computer yako ambacho mtu anaweza kukulipa kufanya?’
Kama huna jifunze. Iwe ni kuandika, kufanya mambo za kutafsiri, iwe ni photo editing, graphics design, video editing, audio production, iwe ni ku code, iwe ni kuongea, kuchekesha, kushauri, kitu chochote.
The more the skills, the better. Na sio mpaka ujifunze ma vitu yaliyo complicated kiivo. Kuko na hii makala inasema kwamba ‘Kama huwezi kufanya mambo makubwa basi fanya mambo madogo kwa ukubwa.‘

So, sio lazima uwe full-stack Graphics Designer, unaweza tu ku focus na kuunda Business Cards peke yake na hicho kikwanndo kitu chako. Na unahakikisha umekua pro kwenye kuunda Business Cards kwanza.
Unataka kuwa unaandika? Sio mpaka ujue kuandika kila aina ya content. Tafuta ninche moja ambayo ina resonate na wewe, ndo ukomae nayo hio hio.
Ni unataka ufanya video editing. Sio mpaka ujifunze ku edit kila aina ya video. Kazi yako inaweza kua tu ku edit video za harusi na masherehe. Na unahakikisha unakua vizuri kwenye hilo. Sio mpaka ujue na kuedit video za miziki, na movie na mambo mambo gani.
Point ya kuondoka nayo kwa hapa. Jifunze kitu. Na kama huwezi kuki master kwa ukubwa wake, basi master ki sub-skill na ukifanye kwa ukubwa.
2. Zingatia Branding

Kua na ujuzi ni hatua ya kuanza ya kuhakikisha una value unayoweza kutoa kwa watu wengine in exchange for money. Branding ndio namna yako ya ku communicate value uliyonayo kwa potential customers.
Branding, ni first impression mtu atakayokua nayo atakapokugundua kwa mara ya kwanza. Kile atakachohisi ndani. Yale ambayo ataweza kujifunza kutoka kwako kwa haraka haraka bila wewe kusema kitu.
Kutokana na namna ulivyojibrand, mtu ataweza determine kama wewe ni mtu serious sana, au uko mchangamfu, kama ni mwelewa au ni authoritative, na kama ni pro kwenye kile kitu unachofanya, au ni beginner. Kama unajichukulia serious, au uko na masikhara.

In short, kupitia Branding, unawaambia watu ni namna gani wakuchukulie. Na Branding sio kuwa na nembo, na consistent graphics, na rangi unazotumia peke ake. Inajumuisha pia, aina ya mambo unayoongelea, unavyoyaongelea hayo mambo yenyewe, the way unavyoandika, the way unavyoongea, the stuff you allow people to see and know about you. Haya yote ni Branding.
So, kua na skills peke yake, haitoshi. Jibrand ipasavyo.
Je unafanya Graphics Design, na una promote designs zako kutumia mitandao kama Behance na Instagram? Swali la kujiuliza hapa hivi ni;
‘Je, ingekua ni wewe unatafuta Graphics Designer na ukakutana na hio Business Page yako, ungeconsider kumcheck mtu husika mfanye kazi?’
Kama hauko sure basi una kazi ya ziada ya kufanya. Hakikisha profiles zako/designs zako/ content zako na kila kitu inayokuhusi ina communicate value yako kwa usahihi. Iwe ni Directly au Indirectly.
Uko na option za kuji brand kama mtu/professional. Au kama Entity/Agency/Organisation. Au vyote kwa pamoja. Which ever it is utachagua, hakikisha umejibrand kisawasawa.
3. Tafuta Approach Sahihi Ya Kujitangaza

Maybe umeanzisha channel yako ya YouTube. Au ni maybe umeanza upload skits zako TikTok. Au umefungua blog na umejibrand uwezavyo. Au labda ni unaenda tumia Instagram…
Changamoto inayokuja most of the time ni kwamba, wewe sio mtu wa kwanza kufanya hicho kitu unachotaka kufanya.
Unataka anza mambo za Social Media Management? Ukiingia Instagram uka search, unaweza ukakata tamaa. Maana utazikuta tayari account zipo nyingi, zina followers wa kutosha nyingine ziko na blueticks kabisa. So unaweza hisi labda umechelewa, au hutopiga hatua.
Maybe umeanzisha Channel YouTube na unafundisha watu wengine mambo ya Music Production. Lakini channel yako ni changa hatari na zipo nyingi zilizokutangulia na zimeshakua kubwa tayari, so swali linakuja; Utaonekaneje?
Jibu ni fupi; Chagua Namna Sahihi Ya Kujitangaza.
Unaweza kua umejinoa wewe na skills zako vizuri, na uko sure sasa ni pro. Na maybe umefanya Competetive Analysis na kuona hao wanaofanya kitu kile unachotaka uanzd kufanya , kipo kitu umewazidi na lipo gap unaweza kupita nalo.

Then umeenda one step ahead, ukajibrand ipasavyo. Umechagua rangi zitakazo respresent brand yako. Umechagua logo yako vizuri. Umechagua your Mission Statement, Vision na umeunda hadi Tagline.
Unajua aina ya watu ambao unataka udeal nao. Umeanza rasmi. Lakini bila kujitangaza sasa watu watakujuaje?
Na kwa hapa hivi issue sio kujitangaza pekee, bali ni unajitangaza kwa namna gani?
Maana kama wapo ma Graphics Designers wengine tayari wenye experience, washajijengea jina na wako na portfolio nene already, nini kitafanya mtu atake kudeal na wewe? Jibu ni Ubunifu.
Ni vizuri kujitangaza in all those conventional ways, kama kuanza ku run matangazo, kuomba co-signs, ku collaborate na watu wengine + kupartcipate kwenye trends.
Lakini ubunifu ni muhimu. Unabidi kua na kitu ambacho wewe peke yako unacho, kitu kitakachokupa ka advantage kuliko hao watu wengine wanaofanya kitu kama chako.
Mfano mwepesi, ni kila mwanaume akogoo na kinyozi wake ambae anamuamini haha. Like asippmkuta huyo ni mara mia asinyoe hadi arudi. Kwanini?
Kwa kua japokua vinyozi ni wengi, anakuwepo mmoja ambaye kwa sababu ambazo hata wewe unaweza usijue, anakupatia tu.
Maybe ni ile attention anayoweka kwenye details, maybe ni kule kukumbuka unavyonyoaga bila kukuuliza kila unaporudi, maybe ni vi ushauri anavyokupa kwa ku suggest mtindo utakaoendana vizuri na kichwa chako. Mambo madogo madogo kama hayo, yanamtofautisha na hao vinyozi wengine.
Labda upo mgahawa unapenda kwenda kula chakula. Migahawa iko mingi. So kwanini unapenda kula pale?
Maybe ni namna chakula kilivyopikwa. Labda huko kwingine hawakuongezeagi mboga za majani, na matunda bure. Labda ni usafi. Au labda kuko na WiFi ya bure.
Mambo madogo madogo kama hayo, yanaweza ku separate huo mgahawa na hio mingine. Hata kama hio mingine imetangulia kuwepo.

Swali linarudi kwako? Uko na nini cha ziada ambacho mtu atapata kwako, amacho hatapata kwingine hata kama huduma ni zile zile?
Hii ndio the most effective way ya kujitangaza bila kuingia gharama. Unatoa ushauri wa kibiashara? Wapo wengine pia wanaotoa ushauri, sasa kwanini mtu aje kwako?
Labda hao wengine hawana blog. Labda hawatoi ushauri wa bure kila kitu kwa ni cha kulipisha. Labda hawakumbukagi majina ya wateja wao. Labda wako slow kujibu. Labda gharama zao ziko juu sana. Labda gharama zao ziko chini sana. Labda hawawapi tu punguzo na tu offer wateja wao. Tuvitu tudogo kama hutu tunatosha kukutofautisha na watu wengine.
So hakikisha, kwa chochote kile utakachoamua kufanya, uko navwo vwa kutosha. Na hii ndio itakua the best approach ya kujitangaza. Maana mtu akipenda huduma. Ako na chance kubwa ya kurudi. Asiporudi ako na chance kubwa ya kukunenea mema kwa wengine ambao wanaweza consider huduma zako.
4. Penda Unachokifanya

Mwanzo ni mgumu. At the beginning unaweza usione matokeo yeyote yale. Effort inaweza kua kubwa lakini huoni kitu chochote kinaendelea.
Maybe video zako zinapata views kidogo na Subscribers wanaongezeka as if hawaongezeki na unataka ku monetize channel yako uanze kuingiza hela.
Au labda unaandika weeeh, mambo mazuri na yenye value ya kutosha lakini hakuna anayesoma.
Maybe unajua designs zako ziko very high quality lakini wateja hupati…Well, uvumilivu unaweza kukuvusha kwenye hii stage. Lakini nayo inaweza isiwezekane, kama unafanya kitu ambacho hukipendi.
Huko juu nimeshauri ujifunze ujuzi unaolipa. Ninachokushauri hapa, ni hakikisha ujuzi utakao uchagua ni ule unao upenda.
Mimi napenda vitu vingi. Napenda kujifunza. Napenda vi challenges and what not. Sio kila mtu anapenda kujua ma vitu mengi. So kwa hayo machache utakayochagua, hakikisha unayapenda.
Upendo wako kwa kile kitu unachokifanya ndio utakuvusha from those hard days ambazo hutokua ukiona matokeo yeyote.
Kama utaamua kuandika, basi hakikisha kua hata wakisoma watu wawili bado utaendelea kuandika. Kwa kua unapenda kuandika.
Napenda mziki. Kama ni issue za kuunda ma beat, kufanya mixing, sound design au mastering. Basi nitaendelea kuzifanya kila nikipata muda. Iwe nimepata clients au hamna. Kwa kua ni hobby nayoipenda.
Hakikisha unapenda unachokifanya, that way hutochoka sana.
Pia Soma: Jinsi Ya Kufanikiwa Bila Kuchoka Sana
5. Anza

Kujifunza ujuzi unaolipa, kuchagua ninche, kujibrand, kujitangaza, kupenda unachofanya, kuwa na mbunifu, na kuendelea kujifunza on the go. Na mambo mengine kibao hayana faida kama hutoanza.
Kama idea yako ni kufungua channel. Ni kua Influencer IG, ni kufungua blog. Ni kuanzisha Podcast, Ni kufanya consultations. Au ni kufundisha kitu fulani kupitia Whatsapp…na izo nyingine zote unazozijua. Hazina faida, kuishia kwenye kupanga, na kuweka mikakati kama hutoanza.
Usisubiri uive. Sijui uwe pro kwanza, au ujue kila kitu ndo uanze. Unaweza kua na idea unique ukahisi wewe pekee ndo uko nayo. Kua unaweza subiri hata miaka miwili au mitano, ndo uanze.
Haha.
Dunia itakushangaza. So anza ivo ivo, na ujuzi ulionao, na kile ulichonacho. Na jiendeleze taratibu. As long as uwe na vision yako kichwani ya aina ya matokeo unayotafuta.
Maybe kwa kuanza, uko na chanches na hauweni kidogo ya ku adapt, kuliko yule anayesubiri.
Pia changamoto ziko nyingi. Baadhi ya ninche ziko saturated sana, kila mtu unakuta ndicho kitu anachofanya.
Kama moyo na skillset zako zinakwambia bado ufanye kitu kile kile, basi kifanye. Haijalishi umekutana na changamoto gani, zigeuze kua masomo na u adapt accordingly.
Ikitokea ukataka kuaza ushindani, basi shidana na wewe mwenyewe. Usishidane na watu wengine. Lengo lako liwe kuhakikisha unajifunza na kua bora na kufanya kile kitu unachofanya kwa ubora zaidi, leo kuliko ilivyokua jana.
Ila sio kukifanya kwa ubora zaidi kuliko fulani. Maana huyo fulani hujui kwanini anafanya icho kitu. Au kaanza na resources gani. Au malengo yake ni yapi.
Shindana na wewe mwenyewe. Ikibidi.
Hitimisho

Hivi ndivyo unaweza kuanza kutumia mitandao kujiajri in a rough sense. Japo yapo mambo ya ziada ya ku consider kwendana na aina ya kitu utakachoanza kufanya.
Kama kitu utakachoanza kufanya kinakulazimu uwe na vibali vya serikali, basi hakikisha uko na necessary documents kuepuka misala isiyo lazima.
Kuhusu kujitangaza sijamaanisha sasa uwe mbunifu kwenye aina na namna za huduma unazotoa kisha utulie. Hamna. Kama bajeti inaruhusu, endesha matangazo.
Jitahidi kila kitu utakacho post, na kuachia, kinaongeza awareness kwenda kwenye brand yako na aina ya value unayotoa.
Na ukifanya hivyo, hakikisha iko clear ni jinsi gani mtu anaweza kukutafuta na kukupata kuanzia mwanzo kabisa na kila kitu iwe simple and straight forward.
Lastly, Jifunze skills za ziada. Kama Emotional Intelligence, Social Skills za Kawaida na Communication Skills. Jifunze Negotiations, na inapobidi Selling Skills.
Zingatia uaminifu, time management, na kusikiliza inapobidi. Good luck.
Discover more from Kainetics
Subscribe to get the latest posts sent to your email.