Kwenye haya maisha ya saa hivi, haswa katika utafutaji, akili inatumika nyingi kuliko nguvu.
Na kama ni kijana mwenye maono na mikakati yake, na ipo sehemu au mahala unataka ufike, na uko na goals/malengo yaliyo serious kidogo unataka uyatimize, basi kuna baadhi ya mambo unabidi uyazingatie sana na baadhi ya mambo unabidi uyakwepe kabisa au kwa muda ili walau uweze kuona matokeo yanayoeleweka.
Kwenye makala hii nitaongelea haya mambo kumi (10) ya kuzingatia kama kijana ukiwa kwenye utafutaji.
Yaliyomo
1. Kua Na Maono (Vision)

Kitu cha kwanza kabisa cha kuzingatia kama kijana ambae anajitafuta, ni kuhakikisha una maono. Maono hai, na yenye uhalisia.
Yaani kabla hujaanza kujiita ‘mtafutaji‘, ‘hustler‘ na kadhalika, unabidi kua sure unafahamu unatafuta nini.
Katika huo utafutaji wako, hakikisha umejiwekea malengo. Na kila kitu utakachokua ukikifanya, itakua ni ku kujaribu kutimiza malengo husika na sio vinginevyo.
Malengo yanaweza kua ya muda mfupi, au ya muda mrefu. Ila uwe nayo. Na kila siku, kila hatua utakayojaribu kupiga ikusogeze kufanikisha malengo husika.
Iwe ni kwenye elimu, iwe ni unajitafuta spiritually, iwe ni kwenye kazi, nk.
2. Hakikisha Una Ujuzi Unaolipa

Kwa lugha nyingine naweza kusema usitegemee sana vyeti. Elimu ya darasani ni nzuri kuwa nayo, lakini hakikisha umejiendeleza kwenye elimu ya mtaani pia.
Na ushauri huo huo unaweza kugeuzwa pia. Hakikisha hutegemei ujuzi/elimu ya mtaani tu. Kua na academic qualifications pia, ni advantage nzuri ya kua nayo.
Ila point ya kuchua hapa, ni kuhakikisha unafahamu kitu kimoja au zaidi ambacho kinaweza kukuingizia hela bila kutegemea vyeti, au elimu yako. (Iwe ni Bachelor, Diploma, Form Six au Darasa la Saba)
Swali la kujiuliza hapa ni; “Nina ujuzi gani ambao naweza kuutumia kujiingizia kipato?” Iwe ni kwa kuajiriwa au kujiajiri.
Labda unaweza kua unajua kuandika, maybe in your spare time umejifunza cartography. Labda unafahamu lugha zaidi ya moja. Au unajua cheza na computer kisawa sawa. Au simu.

Au labda uko vizuri kwenye problem solving na kutoa ushauri. Labda umejifunza na unafahamu namna ya kutumia camera. Au unajua namna ya kuunda graphics. Kuendesha gari. Pikipiki.
Coding. Ethical Hacking. Kitu chochote ambacho mtu anaweza kukulipa kufanya. Iwe ni kipaji au ni kitu umejifunza. Ila hakikisha una ujuzi wowote ule unaolipa.
3. Soma Sana Vitabu

Sio kila mtu ni mpenzi wa kusoma vitabu. Ila kila mtu anafahamu kwamba ili mwili huweze kufanya kazi ipasavyo basi inabidi ule. Na sio kula tu, ule chakula chenye nutrients za kutosha ili uweze kuendelea kua na afya iliyo bora.
The same, ina apply kwenye bongo zetu. Ili uweze kua na mawazo makubwa, uweze ku improve problem solving skills, ubunifu wako, social skills, the way una percive mambo, nk. Lazima ujiexpose na Big Ideas.
Na Big Ideas hizo sana sana utazikuta kwenye vitabu. Hivyo unabidi kujiwekea desturi ya kusoma hivyo vitabu vyenyewe, hata kama sio mpenzi sana wa hayo mambo.
Kila mtu lazima ale, hata kama sio mpenzi wa kula.
Hivyo basi, jitahidi mara moja moja, more often than not, kuhakikisha kwamba unasoma na kujifunza kitu kipya. Kama sio mpenzi wa kusoma na hata ujilazimishe vipi, unajua huwezi. Basi unaweza tumia medium tofauti.

Maybe consider Audiobooks. Au tafuta Book Summaries. Na kama unajifunza vizuri zaidi kwa kutazama, basi hakikisha watu unao wafollow ni wale wanaotoa madini, na kufundisha mambo ya maana. Point kubwa hapa ni kuhakikisha unakua mtu anayependa kujiendeleza kwa kujifunza mambo mapya.
4. Jitahidi Kua Na Connection Za Maana

Kwenye dunia ya sasa, thamani yako, na uwezo wako wa kuvuka au kujiboresha kwenda hatua nyingine, iwe ni ndogo au kubwa, kwa namna moja au nyingine, inategemea na unafahamiana na nani.
Hivyo, jitahidi kuhakikisha unazungukwa na watu wa maana, watu wanao ku inspire na kuku challenge kua bora zaidi, kila siku.
Zungukwa na watu wanao waza tofuati, wanaofanya mambo tofauti, au mambo ambayo unatamani kufanya ili uweze kufahamu wanayafanyeje.

Kua na watu ambao unaweza ongea nao mambo ya maana kidogo, kubadilishana mawazo, kupeana deals zenye manufaa, watu ambao mnaweza saidiana kwenye majanga, watu wanao kuelevate na kukutoa usingizini.
Na sio kuzungukwa na watu ambao mnakutana kujadili mambo yasiyo na tija, kujadili watu wengine, udaku, na mambo kama hayo.
Hapa simaanishi uwe parasite. Hakikisha pia na wewe ni mtu ambae anaji challenge mwenyewe na unazidi kujiboresha kuhakikisha una value pia unayoweza kutoa.
Kama labda unataka uwe kwenye circle ya mtu fulani, swali la muhimu kujiuliza kwa hapa ivi ni “Je, yeye atataka kua kwenye circle yako pia?”
Kama jibu ni hamna. Basi uko na kazi ya kufanya kuhakikisha uko na value ya kutoa kwa watu.
5. Usiwe Mshamba Wa Hela

Kwa Kingereza ningeandika kwamba uhakikishe uko “Financially literate”.
Kutafuta hela, ni swala moja wapo, lakini namna ya kuzimeneji, kuzitumia, na hata kufanya zikuingizie hela nyingine ni swala jingine tofauti.
As I write this, utakuta kuna sehemu huko somewhere, kuna mtu anaingiza laki na nusu tu kwa mwezi, ila amefanikiwa kujenga, na anasomesha watoto. Familia yake inakula vizuri na wanavaa, maisha yanaenda.
Upande wa pili, utakuta kuna mtu anaingiza laki nane kwa mwezi lakini bado haitoshi, kufanya hata yale mambo madogo madogo na kumuendesha kwenda mwezi mwingine.
Huu ndio nauita ushamba wa hela. Kitu cha muhimu kujifunza hapa ni “Living within your means.“

Yaani, kuhakikisha matumizi yako hayazidi 80% ya kipato chako. Maana asilimia kubwa ya matatizo yasiyo ya lazima, yahusuyo hela, hutokana na watu kutaka kuishi maisha yasiyo ya kwao.
Hivyo ishi maisha yako. Na sio maisha feki. Kama kipato chako hakiruhusu kupangisha chumba cha laki mbili na nusu kwa mwezi, usilazimishe. Hata kama wenzio, umri sawa na wewe, wanafanya hivyo.
Kama kipato chako hakikuruhusu kuvaa saa ya laki nne na nusu, usiforce mambo. Zipo saa za elfu tano na zinaonesha muda ule ule. Live within your means.
Kama nilivyosema hapo juu, kujifunza kutafuta hela ni kitu kimoja. Ila kujifunza kuitumia hio hela vizuri, kuweka akiba, na hata kuwekeza ili ikuingizie hela zaidi ni kitu kingine entirely.
Na ukizingatia icho, na ukajifunza na kujizoeza ivo (hata kama inaweza kua ngumu mwanzoni) basi utakua umeshapiga hatua kubwa maana mambo mengi huanzia kichwani. Ukiweza kua vizuri kichwani, financial-wise, basi lazima uone matokeo. Maana umaskini, unaanzia kichwani. Hivyo kichwani huko ndiko sehemu ya kuanza nako.
6. Jizoeze Kukataliwa

Kuko na watu wengi huko ivi, wanaogopa kutoa mawazo yao, kuonesha walicho nacho, na kujaribu fursa mbali mbali, kisa tu wanaogopa kukataliwa.
Wapo watu wanaogopa kutuma maombi ya kazi, au ku attend interviews, nk. Kwa kua wanaogopa rejection.
Usiwe mmoja wao.
Kama ni kijana mpambanaji, itabidi ujizoeze huko kukataliwa. Maana kwa ninavyoamini, kabla ya mlango sahihi kufunguliwa, lazima utafungiwa milango mingi.
Utarudishwa nyuma, utachekwa, utadhihakiwa mwanzoni, utaambiwa hapana, utanyimwa fursa kibao, lakini hizi changamoto hazipaswi kukukataza kuendelea kujaribu.
Bali zinabidi kukusukuma, na kukutia moyo, kujua kua ipo kitu huko inakusubiri, na hutoifikia/kuipata au kujua kama ndio ilikua kitu sahihi, kama utakua muoga kujaribu kisa tu unaogopa kukataliwa, au mambo kufeli.
7. Jitangaze. Jitangaze. Jitangaze

Wapo watu wengi mno, wana vitu vikubwa, vipaji vikubwa na wako vizuri kwenye vitu wanavyofanya lakini hawajulikani kwa kua hakuna namna ya kuwajua. Kwa kua hawajioneshi.
Unaweza kua uko vizuri kwenye mambo za kuchora. Ila mtu bila kuona michoro yako atajuaje?
Unaweza kua ni mwandishi mzuri tu. Au labda unajua kuimba. Ni MC. Ni mchekeshaji. Maybe ni Web Designer kama mimi, or Programmer, au ni Producer, unajua mwenyewe…ila kama hujaambiwa watu kua uko vizuri kwenye sekta hio hakuna namna watakujua.
So, jitangaze. Tuko kizazi cha kidigitali, kufungua account ya TikTok, Instagram iwe ni Channel ya Youtube, Tovuti, nk. Ni kitu ambayo inawezekana.
So tangaza fani/ujuzi wako kwa namna yeyote unayoweza. Iwe ni kupitia word of mouth, ni kwa kupost picha, reels, au kuandika. Jitangaze.
Huwezi jua nani atakua anaangalia. Maybe yupo mtu huko hivi anamtafuta mtu kama wewe. Ila bila kujitangaza. Hatokupata. So, ambia ulimwengu unafanya nini.
8. Nguvu Kidogo, Akili Nyingi

Kwenye kitu chochote unachofanya, always tafuta namna ya kukamilisha mambo kwa kutumia akili na sio kujitesa. As long as unayafikia matokeo uliyokua unayatafuta.
Usipende kua busy tu, ilimradi uonekane uko busy, bali hakikisha huo ubusy wako una matunda.
Kama uko na kazi unabidi uifanye, na unafahamu kwa kawaida itakuchukua masaa 10 kuikamilisha. Chances ziko kubwa kua kuna kitu unachoweza kufanya kupunguza huo muda, hivyo usiache kuvitafuta vitu ivo na kuvi encoporate kwenye kazi zako.

Mbali na kuokoa muda, tumia principle hio hio kuokoa hela. Kama kuna kitu kinabidi kifanyike na kinahitaji hela, jitahidi kumake sure kwanza kua hakuna namna unavyoweza kupunguza gharama husika, au kukifanya hata bure as long as kitaleta matokeo yale yale unayoyatafuta.
Kwa kufanya hivyo, utaokoa muda wako mwingi, wa wateja wako. Hela yako, pamoja na hela ya mteja kitu ambacho kinaweza kufanya upewe kipaumbele kwenye kazi zijazo.
9. Kumbuka ‘Uaminifu Ni Mtaji’

Kwenye mapambano na mahangaiko yako kama kijana, zingatia kitu kinachoitwa uaminifu na jitahidi kuepuka kona kona.
Hii itakusaidua sana kwenye namna ambazo hata wewe unaweza usijue.
Haijalishi utakua unafanya kazi gani, jitahidi tu kuhakikisha uko mkweli na muwazi kadri uwezavyo, maana kwa dunia ya sasa uongo na udanganyifu uko mwingi sana. Hivyo kwak ua mkweli, na muwazi, unajipa advantage ambayo wengi wanakosa.
Kama kipo kitu x kinaweza kufanyika kwa ukamilifu kwa shilingi laki tano. Hakuna sababu yeyote ya maana ya kudanganya na kusema kinafanyikaga kwa laki saba.

Kama kitu unao uwezowa kukifanya bure unakifanya. Na kama kinafanywa kwa gharama, lakini ipo alternative ambayo ni cheaper, basi make sure hio alternative inajulikana.
Jitahidi kua muwazi tu kwa watu wanaokuamini na kukupa kazi, maana at some point, huo huo uaminifu, ndio unaweza kua kigezo pekee kitakachofanya uwe considered.
Hivyo naweza ku conclude hapa ivi kwa kusema , uwe muaminifu. Maana uaminifu ni mtaji.
10. Jifunze Uvumilivu

Wapo wengi wanaokua na ideas unique, na wanazianzisha lakini ideas hizi nyingi huishia njiani kwa sababu waanzilishi wake waliwahi kata tamaa.
Kwenye makala yangu inayoongelea jinsi kuanzisha blog, nlisema blog zipo nyingi zinazofunguliwa na kuanzishwa kila siku, lakini zinazoendelezwa ni chache. Maana watu wengi wako na mentality ya kuona matokeo kwa haraka hivyo wasipo ona hukata tamaa na kughairi kuendelea.
Hii haiko kwenye swala la blogging tu. Hata kwenye biashara. Maduka, makampuni, migahawa, na mahoteli hufunguliwa kila siku, ila wale wanaoweza kustahimili kipimo cha muda ni wachache mno hivyo biashara nyingi unakuta zinaishia njiani.
Hivyo basi, kwenye kitu chochote kile utakachofanya. Jitahidi kua mvumilivu. Na kuelewa kwamba vitu vizuri havihitaji haraka.
Hitimisho

Kwenye makala hii nimeongelea mambo mengi, tofauti tofauti, mambi ambayo hata mimi najitahidi niwezavyo kuendelea kuyazingatia na kuyaheshimu hivyo natumai kwa namna moja au nyingine kwa yeyote ambaye atapitia anaweza kuondoka na mawili matatu pia.
Kitu cha mwisho nachoweza kuhitimisha nacho, ambacho kimeongelewa kwa kina kidogo kwenye makala hii nliyosoma siku kadhaa nyuma, ni kwamba tunapokua kwenye huu utafutaji tusisahau kuishi.
Mara moja moja jitoe out…kula vizuri. Vaa vizuri. Tembea. Usikate mawasiliano na watu wanaokujali na kukutakia mema. Usisahau kupumzika. Kuji enjoy inapobidi. Na usisahau pia kuomba. Karibu.
Discover more from Kainetics
Subscribe to get the latest posts sent to your email.
Upo sahihi sana