Moja ya kikwazo kikubwa kinachotuface kama watanzania ikija swala zima la kujiajiri mtandaoni, iwe ni kwa kufanya Freelancing au Affiliate Marketing au issue yeyote itakayokutaka kupokea pesa kutoka nje ya nchi, ni kwamba PayPal kwetu hairuhusu kupokea malipo, bali kutuma tu.
Ila hii isikukatishe tamaa, kwenye makala hii nitaongelea njia tatu mbadala unaweza kutumia kupokea malipo mtandaoni.
Ukiweza kusoma hadi mwisho kabisa, kama bado unatamani kuwa na PayPal inayoweza kutuma na kupokea pesa, nitakuelekeza ni namna gani unaweza kufanya hivyo japo ina gharama kidogo.
Bila kupoteza muda, tuanze;
1. Grey

Kama unatamani option nyepesi zaidi isiyo na longo longo nyingi ambayo unaweza kutumia kupokea pesa kutoka nje ya nchi, na kuitoa directly kwenda kwenye account yako ya Bank ya kiTanzania, basi consider kutimia Grey.
Haina mambo, mengi na inakuruhuzu kufungua account yako kama una kitambulisho cha NIDA, Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au Passport.
Ukishafungua account, grey itakuwezesha kua na account inayopokea pesa za kigeni iwe ni USD, au EUR. Na hizi unaweza kuzitumia kupokea pesa bila tatizo lolote.
Kufungua account ya Grey, gusa HAPA.
2. Payoneer

Option nyingine nzuri isiyo na longo longo ambayo utaweza kutumia kupokea pesa kutoka nje ya nchi basi ni Payoneer.
Hii iko na Advantage ya kwamba inatambulika na Freelancing sites kadhaa, hivyo ukiwa na account ya Payoneer unaweza kuiunga directly na Fiverr, UpWork, People Per Hour au Freelancer.
Unachohitaji kufungua account ya Payoneer ni uwe na kitambulisho cha aina yeyote kinachodhihirisha kua kweli wewe ni mtanzania. Mfano;
- NIDA
- Leseni ya Udereva
- Passport
Pia utahitaji kua na account ya Bank inayofanya kazi. Ambayo utakua ukitumia kupokea hela kutoka Payoneer.
Pia, wako na Card yao maalumu ambayo unaweza omba, na kutumiwa ambayo utaweza kutumia kutolea hela kwenye ATM yeyote ile nchi yeyote ile.
Nimeiweka nafasi ya pili kwa sababu makato yao ni makubwa kidogo, huvyo jitahidi wakati unatoa hela kiasi cha pesa ambacho utakua unatoa, kiwe $60 au zaidi.
Kujiunga na Payoneer, gusa HAPA.
3. Skrill

Namna nyingine ya uhakika unayoweza kutumia kupokea malipo mtandaoni ni hii Skrill.
Hii haina longo longo nyingi, na namna zao za kufanya verification ziko tofauti kidogo.
Kwa Skrill, hauhitaji kua na kutambulisho cha aina yeyote japo ukiwa navyo ni vizuri zaidi kuraisha process ya verification.
Unaweza kuverify account yako, kwa ku deposit kiasi kidogo cha fedha cha $1.
Na ukiwa umesha verify namba yako ya simu pamoja na email, tayari unakuwa umemaliza na kuweza kuanza kutumia account yako kwa ukamilifu wake.
Skrill kwenye Freelancing Platforms sana sana hutoikuta imeungwa kama namna moja wapo ya kupokea malipo, hii utaikuta kwenye sites za Affiliate Marketing, Brokers wa Forex na sites za kimataifa za Kubet.
Hivyo, unaweza ku consider kutumia hii kama clients wako mnapeana kazi moja kwa moja bila kupitia kwenye izo Platforms.
Kujiunga na Skrill, gusa HAPA.
4. Nyongeza: Direct Bank Transfer

Ipo option ya kupokea malipo directly kwenda Bank kama una sababu nyingine nyingine zinazokuzuia kufungua izo e-wallets.
Platform baadhi za Freelancing, Affiliate Marketing, nk zinaruhusu kupokea malipo yako kwenda Bank moja kwa moja, japo njia huu uchelewa kidogo kuliko izo nyingine kwenye kupokea malipo yako.
Muda mwingine huchukua siku 5 hadi 10 hela yako kusoma; Ila hela husoma.
5. Account Ya PayPal Ya Nje

Kama bado ulikua unatamani uweze kuoata namna ya kutumia PayPal hio hio kupokea malipo kwa kua huwa ndio njia rahisi zaidi isiyo na longo longo, na pia huwa mimala yake huwa ya papo kwa hapo, basi unaweza consider kufungua account ya PayPal iliyotengenezewa nje ya nchi.
Kama una rafiki yako ambayo anaishi nje/kwenye nchi inayo support kutuma na kupokea pesa… Basi unaweza muomba akusaidie kukufungulia account.
Pia, unaweza fungua account ya PayPal ya Kenya, kama utaweza kupata mtu wa kukusajilia namba ya simu ya Safaricom. Ukiwa na hii inamaanisha hela yako iliyo PayPal utaweza kuituma kwenye hio namba yako ya Safaricom na kisha kujitumia kwenye namba yako ya Tanzania.
Kama unahitaji kufunguliwa account ya PayPal ya nje iliyokamilika kwa ajili ya kupokea malipo, waweza nicheck.
Gharama ni Tsh.200,000/- kama utahitaji account iwe kwenye majina yako.
Na Tsh. 85,000/- Kutengenezewa account iliyoungwa na Line ya Safaricom (Line pia unapewa.)
Kunicheck, Gusa Hapa.
Hitimisho
Hizo ndizo namna za uhakika unazoweza kutumia kupokea pesa kutoka nje ya nchi kama mbadala wa PayPal kwa sisi waTanzania wenye harakati mtandaoni.
Kumbuka kuzingatia mambo mengine ya kawaida, ila ya muhimu kama kuhakikisha wakati unafungua izo account, basi ;
- Utumie majina yako halisi
- Link namba yako ya simu
- Link na verify email yako
- Usitumie account zako kwa issue za kitapeli na mambo mengine kama hayo
Karibu!
Discover more from Kainetics
Subscribe to get the latest posts sent to your email.