Habari, kwenye hii makala ya leo nitajaribu kutoa ushauri deep kidogo kwa wale wanaotaka kuanza kujiajiri kutumia mitandao kwa huu mwaka wa 2025.

Every now and then, huwa napokea sms/maswali yanayolihusu swala hili kutoka kwa wadau ambao hupitia makala zangu— sana sana kutoka humu kwenye blog— na wengine kutoka kule JamiiForums na huko kwingine ambako huwa naandika nikipata ka nafasi.

Swala la kuombwa ushauri kuhusu jinsi gani mtu anaweza kuanza kujiajiri mtandaoni, ni kitu nakua naulizwa mara kwa mara, na ndio sababu niliandika ile makala iliyopita;

Makala Yenyewe: Jinsi Ya Kutumia Mitandao Kwa Usahihi Na Kuanza Kujiingizia Kipato

Humo nliongelea yale mambo ya msingi na muhimu kabisa, kama kuhakikisha una ujuzi unaolipa, Kuzingatia Branding, Kujitangaza na hatimae Kuanza.

Kwenye makala ya leo siendi kurudia mambo yale yale ambayo tulishaelezana kwenye hio post. Instead; humu nitaongea na wale wanaoanza rasmi.

Lengo likiwa kuelekezana na kushauriana baadhi ya vitu, according to my own personal experience. Bila kupoteza muda wa ziada, tuanze;

Utangulizi: Mimi Na Ushauri Wapi na Wapi?

Snaposhot ya Leo | Moja ya Store zangu/Shopify

Haha, hii title bado inanichekesha. Anyways, likija swala la ushauri kama ambavyo nimekwisha sema hapo mwanzoni, ushauri huu nautoa kwa wale ambao wako na ujuzi tayari wa aina yeyote ile, na wamefanya research zao na kujiridhisha kuwa wako tayari kuanza safari zao za utafutaji online.

Mimi ni nani kutoa ushauri? Sidhani kama hili ni la muhimu kiivyo. Ila kama ndio mara kwanza umeingia kwenye blog yangu na hii ndio post ya kwanza wewe kufungua, well, naitwa Frank.

Nimekua niki hustle na hizi mambo za mtandaoni toka tangu na tangu, na kwenye hii miaka michache ya kuhangaika (iwe ni kama Freelancer, Blogger, Programmer, Graphics Designer, Full-Stack Developer, Editor, Forex Trader, Web Designer, Tutor, mwana E-commerce, na mambo mengine kibao…) naweza sema nimekutana na kila aina ya rangi, haha.

So mambo mabovu na ya kiwaki unayoweza kutana nayo online, nadhani most of them vimenikuta.

documents on wooden surface
Photo by AS Photography on Pexels.com

Sijatoboa bado haha, ila pia naweza kusema na mazuri pia, kwa asilimia zake, nimekutana nayo.

That said, yote nitakayoongelea humu ni yale tu nliyo experience first hand. Na lengo ni kupeana mwanga na kuraisishiana safari (maana posts zinazoongelea hizi mambo kwa Kiswahili na kwa upana kidogo nadhani hazikuwepo so our journeys had to be through trial and error. Ila haipaswi kuwa hivyo sasa.)

So, iwe umeamua unataka uwe YouTuber, au maybe ufungue blog ui-monetize kwa matangazo, au labda na wewe ni Web Designer kama mimi na unataka uanze kuundia watu websites, au maybe unataka ufungue Online Store

Chochote kile utakachokua umechagua, as long as ni unafanya kwa malengo ya kuhakikisha kitu husika kinakuingizia hela, na value yako ionekane kwa watu sahihi basi natumaini utaweza kupata kitu au viwili.

1. Branding Kwa Kina

Baadhi ya Analytics za hii blog ya Kainetics

Kwenye hizo makala nyingine, nilishazungumzia swala la kuingiza pesa mtandaoni kwa njia za uhakika na zisizo sua sua, unaweza kulifanikisha either kwa kuuza kitu/huduma au u monetize content zako.

Pia Soma: Namna 37 Za Uhakika Unazoweza Tumia Kujiingizia Kipato Mtandaoni Kwa Mwaka 2025

Zipo njia nyingine kama mambo za Kutrade Forex na mambo za Cryptocurrency ambazo hazifuati hio sheria hapo juu, lakini ili uweze kufanikisha hizi ni mpaka uwe na mtaji unaoeleweka na pia uwe unaelewa unafanya nini.

Sema sio kila mtu ako na mtaji wa maana na uelewa wa hayo mambo that’s why sitoziongelea in deep kwenye makala hii.

Nirudi kwenye point;

shallow focus photography of pepsi cola bottle cap
Photo by Izabella Bedő on Pexels.com

Kwenye hizo hizo makala za nyuma, ipo makala niliyoongelea mambo za Branding kiufupi. Na nadhani nlisema kwamba kabla hujaanza kujiajiri online, utabidi uchague ujuzi wowote utakao kuingizia hela, lakini nikasisitiza kua ujuzi pekee hautoshi, itabidi uji brand kwa usahihi, kama utataka kuchukuliwa serious kwenye kile kitu utakachokua umeamua kufanya.

Na hapo hapo kwenye branding nilisema mwanzoni kabisa unaweza kuamua kama utafanya kazi na kuji present as an individual or entity.

Individual/Personal Branding

Mfano; Wote ambao tumefanya kazi pamoja, wanafahamu kua wamefanya kazi na Frank, na sio Kainetics japo kua Kainetics wana ihusisha directly na mimi.

Client wako akiweza kuoanisha ujuzi ulionao na jina lako, basi kwa asilimia kadhaa unakua umeifanikisha hio personal branding as a thing.

Yaani mtu kukutafuta akijua fulani—let’s say unaitwa John—kua John ni Graphics Designer. Tayari unakua umefanikisha kujibrand as a person. Kwa ufupi.

Branding As An ‘Entity’

Upande wa pili, unaweza kuji present as an entity/kikundi/kampuni/etc. Hapa kinachotokea ni kwamba ujuzi wako na kile kitu unachokifanya, hakioanishwi na wewe moja kwa moja as a person, bali jina la Kampuni/Entity/’Brand‘ yako.

Ukifanya aina hii ya Branding basi mteja hatokutambua as a single person, bali as a body. Yaani utakua addressed kwa wingi na sio umoja. Na kujibrand kwa namna hii kuna make sense kama kazi utakazokua unafanya utakua unazifanya na watu wengine, au zinakulazimu ku act as an agency ili uweze kupata baadhi ya tender/mikataba.

Nikirudi kujitumia kama mfano, zipo baadhi ya kazi ninazofanya, ambazo wateja hawanitambui kama mtu mmoja, bali wakiwa wana address kazi/project husika wanaweza sema kitu kama ‘Hii kazi inafanywa na Kainetics.’

Na ikiwa hivyo most of the time, inamaanisha kazi husika naifanya na team ya watu wawili au zaidi ili kumeet deadlines na muda mwingine kutoa matokeo yanayohitajika.

close up photo of camera lens
Photo by Lukas Hartmann on Pexels.com

Hivyo basi, chagua utafahamika vipi, kwa jina la Biashara yako, au kwa jina lako binafsi? Au vyote kwa pamoja? Na hakikisha kwa chochote utakachochagua uta kibrand accordingly.

So far, ukifumba macho ukaulizwa ukisikia neno ‘Vodacom‘ nini kinakujia kichwani…well, inategema. But majibu ya wengi yataoanisha rangi nyekundu na hilo neno. Wengine wataonanisha hali ya ‘uhakika/kutobabaisha’ na hilo neno pia. Hio ndio nguvu ya Branding.

So kuchagua the way utakavyofahamika haitoshi, unabidi uamue pia utafahamiwa kwa yapi? Unaongeaje, unaongeleaga nini? Kazi zako zina ubora gani? What’s your story? Are you formal au uko casual? Sawa mnaitwa GadTrix ila mtu akisikia hilo jina; anaoanisha sifa gani na brand yenu?

Hayo ndio mambo ya kuzingatia kwenye kujibrand…mwanzoni kabisa mwa safari yako. Na tukiwa hapo hapo kwenye hilo swala la ‘kufahamiwa’, twende kwenye point ya pili;

2. Chagua Kimoja Kwanza: Kutengeneza Jina au Kulipwa

Store hii ni ya kuuza Beats/Sample Packs | Shopify

Ushauri mwingine wa muhimu kidogo ninaoweza kutoa kwa mtu anaeanza safari yake ya kujitafutia kipato online, ni huu;

Chagua Kimoja Kwanza. Kama Unataka Ujitenegenezee Jina au Unataka Ulipwe/Uingize Hela.

Branding ni muhimu, kwa biashara ya aina yeyote ile. Na kama unaenda fanya mambo yako in a professional sense, ni kitu ambacho unabidi ukizingatie.

Ila sasa, kwenye kukizingatia kwenyewe, zipo njia mbili unaweza kupita; Either u focus kwenye kujenga Awareness ya Brand yako na kupitia hio upate kazi, more prospects, utanue portfolio na CV yako…

Au, u focus kwenye kujiingizia pesa kwanza, hio Brand ikufuate. Haya ni mambo mawili tofauti, na ni kitu unachobidi uamue, mwanzoni kabisa mwa safari yako ya utafutaji.

Niko naongelea nini?

person using laptop on gray table
Photo by HARSH on Pexels.com

Well, ngoja tueleweshane kidogo;

Kama uko unasoma makala hii kwenye blog yangu, then kuko na uwezekano wa asilimia kadhaa kua kuna kitu ulikua una Google kinachohusiana mambo haya haya, na hivyo ndivyo ulivyokutana na makala hii. Jina Kainetics. Na jina Frank. Na kabla ya hapo, hujawahi kuniskia mimi na blog yangu kama tuna exisit.

Upande wa pili, maybe hio scenario ndivyo ulivyonifahamu, ila haijatokea kwa post hii, ni kwa post nyingine tofauti. Au maybe haikua kwenye hii blog, maybe thread ulikutana nayo JamiiForums.

Kama umenifahamu kwa njia izo, basi umenifahamu kupitia Jina— na hii simple Branding ya Kainetics.

Lakini hii blog ni changa. Ina miezi kama minne hivi toka niianzishe, na project hii ya Kainetics ilianzia Jamii Forums. Niko nina muda toka niandike kitu kipya huko. Makala Ndefu Ndefu nlizoachia nadhani kwa mara ya mwisho ilikua 2022.

So, kama ninasema ninafanya kazi zangu online, na muda wote huu hapo kati kati nlikua dormant (kwenye public net), ko ina maanisha nlikua sifanyi kazi?

Snapshot ya Leo April 16th | Shopify

Haha. Hamna. Nimekua nafanya kazi hizi hizi kabla hata sijaanza kuandika huko JamiiForums. Kabla sijafungua blog ya Kainetics kwa mara ya kwanza 2022, na kabla sijaifungua tena kwa mara ya pili mwaka huu 2025.

Ila muda wote huu, barabara niliyochagua, ni hio ya Kulipwa.

Na kama ni mtu ambaye yuko serious sana, na mambo hayako vizuri kiivo in all aspects wakati unaanza, (maybe huna hela za kuanza ku run matangazo, na kujibrand ipasavyo) then kitu nachoweza kukushauri ni Chagua Kulipwa Kwanza.

Huko Kulipwa Kwenyewe Kukoje?

black and white box beside white metal rack
Photo by Nataliya Vaitkevich on Pexels.com

Well, kama ni kui summarize hii point, basi naweza sema usitake kujulikana, au kua credited kwenye kila kitu au project utakayofanya. Wewe kitu cha kuzingatia ni kuhakikisha umelipwa na ubora wako umeonekana. Basi.

Toka mara ya kwanza nianze kuunda tovuti, nimeunda tovuti kibao mno, kwanza nikiwa kama this unexperienced dude ambae hata hajafikisha miaka 18, then kama Freelancer huko Upwork (kwa clients wa nje) na taratibu nikaanza kuunda zile za clients wa kitanzania. Mambo za Graphics Design, Branding, SEO, na hiyo mi vitu mingine yooote, nimewafanyia watu wengi tu, na hio kuwafanyia kazi zao kwa ubora, kwangu inatosha aa long as wamenilipa.

Mambo ya kujulikana kua fulani ni client wangu, au mimi ndiyo nliye unda kitu fulani, hayasaidii kiivo. Though every now and then ninaweza share baadhi ya kazi zangu za nyuma na potential client, ila sio rahisi.

Kwa kazi yeyote ile nitakayomfanyia mtu, huwa siachi any of my branding in any way

(eg. Tovuti hii imeundwa na Kainetics. Au kuweka nembo yako kwenye kazi za mteja, nk.)

Ukiwa una act kama Brand, hizo zinaweza kuwa njia nzuri za kujipa exposure, ila itakuweka at a disadvantage kama unaanza. Maana nimesema moja ya malengo muhimu ya hizo Branding ni kuamua unahusishwa na aina gani za kazi.

Ukichagua kulipwa, na kutokua credited, well hio inakupa freedom ya kufanya kila aina ya kitu unachoweza kufanya ili mradi uingize hela.

photo of person holding smartphone
Photo by Anna Nekrashevich on Pexels.com

Na kwa kufanya hivyo unaweza experiment na aina tofauti tofauti za kazi kama ujuzi wako unaruhusu…hadi upate kazi zile utakazoona zinakufaa na uko tayari kuji identify nazo.

That said, nimefanya sana mixing na mastering za nyimbo za watu haha, lakini anaejua kua nimefanya izo mambo ni wale waliokuwa wakinipa hizo kazi, nao wananitambua kama Producer. Wapo wanaonijua tu kama mchoraji, na wapo wanaonijua kama jamaa wa SEO, na wapo wanaonijua kama jamaa wa Ads, jamaa wa IT, Graphics Designer au labda Web Designer.

Na kati yao, wapo ambao hawajui kuwa nilikua nafanya hivyo vitu vingine roughly at the same time, na wapo wachache ambao wananifahamu kwa hivyo vitu vyote kwa pamoja.

Hii Kainetics ndio blog yangu peke iliyo kwa Kiswahili, na ndiyo blog yangu pekee ambayo unaweza kuihusisha na mimi moja kwa moja.

Ila zipo blog nyingine ambazo nimeanzisha tangu na tangu ili ziingize hela, basi. Sio mambo za kufahamika au kujulikana kwanza. Zipo channel za YouTube Faceless zilizoanzishwa kwa madhumuni hayo. Zipo store za E-Commerce. In short vipo vitu vingi vilivyoanzishwa kwa madhumuni ya kuingiza hela na sio vinginevyo.

Na kama ni mtu ambaye yuko serious, basi naweza kukushauri focus na mambo yatakayokuingizia hela kwanza. Na sio ujulikane.

Baadhi ya Earnings zitokanazo na Dropshipping

Usichague kazi. Jikite na Ninche tofauti tofauti (fungua blog ikibidi kwa ajili tu ya Adsense, fungua Channel hata kama content husika hazihusiani na mambo yanayokuhusu ili mradi iwe monetized na iwe inaingiza hela…whatever it is you can do, that’s legal and scalable; Do it)

Hao wachache watakaokufahamu along the way wanatosha.

Na ikifikia stage, hio kufahamika ikawa ni factor muhimu, basi utakua na experience tayari ya kujua nini kinafanya kazi, na nini hakifanyi kazi. Nini kina lipa. Na nini hakilipi. So, utaji-brand, accordingly.

Na kwa kua bado tunaongelea branding, na kuingiza hela twende kwenye point ya tatu;

3. Chochote Kile Utakachofaya, Kifanye Kwa Ubora Wa Asilimia Mia

Idadi ya Subs kwenye Blog yangu nakofanya Affiliate Marketing

Haijalishi ni kazi ya shillingi elfu kumi, au ni kazi ya laki tano, ni kazi ya million mbili…Kazi yeyote ile, iwe ni kubwa au ndogo, hakikisha umeipa asilimia zako 100%

Hakikisha kwa ule ujuzi ulionao by the time unaikabidhi uwe umeridhia na nafsi yako kua kwa ninavyoweza, hii kazi nimeifanya kikamilifu.

Sema hapo hapo, kwenye kufanya kazi kikamilifu, huwezi kufanya kazi yeyote ile kwa asilimia mia kama huipendi.

Hivyo chagua vizuri kazi utakazo kubali kuwafanyia watu. Iwe wewe ni Web Designer, au uko vizuri kwenye Content Strategy, au labda uko vizuri kwenye mambo za Voice Over, au maybe ni mtu wa ku code… project yeyote ile utakayoipokea, hakikisha ni project ambayo unajua unaenda kuipa asilimia zako zote.

Hii itakusaidia kuhakikisha portfolio yako haina kazi mbaya mbaya au hafifu kuanzia mwanzo kabisa. Na ikitokea kazi ya nyuma ukaiona iko hafifu now. Basi uione ivyo kwa kua kwa sasa kuna vitu unavijua ambavyo ulikua hujui wakati huo…na sio kwa kua kazi uliifanya kimasikahara.

Unachaguaje Project Kwa Usahihi?

close up photo of a person using laptop
Photo by Edmond Dantès on Pexels.com

Well, kwa kuhakikisha kua you can meet all the requirements kazi husika inahitaji.

Kitu kingine ni kuhakikisha umeridhia na kiasi cha fedha utakacholipwa, pamoja na utaratibu mzima wa malipo yenyewe.

Pia zipo factor za ziada unazoweza ku consider ikiwemo uelewa wa client husika na vitu anavyojaribu ku achieve.

Maybe watakuwepo baadhi kwenye wanaosoma makala hii waliowahi nicheck tufanye kazi fulani, haswa wa kuunda blog…na gharama zikawa sio shida, ila baada ya kuulizana maswali mawili matatu nikaikataa kazi husika, na maybe kushauri mhusika akaongeze ufahamu wake na kitu husika ili aelewe kwanza analipia kufanyiwa nini, na nijue kwamba hii blog/tovuti nikiipa asilimia zangu mia basi zianenda kutumika kwa usahihi. Mbali na hapo ni heri kazi inipite.

UpWork Connects hutumika wakati wa kuomba kazi

Hii inadepend na utakua unafanya kazi za aina gani. Lakini kama kazi husika inamfanya mteja awe dependent kwa skills zako, basi the best policy ya kutumia ni kuhakikisha anaelewa the whole scope ya mambo ambayo yako within your range kutimiza. Na mambo gani sio majukumu yako, mbali na hapo mtazinguana sana haha.

Kwa kutumia huo huo mfano wa kuunda blog, utakuta mtu anataka umuundie blog kwa kua ameona screenshot yako ya mapato yako Adsense kwenye status then aka assume moja kwa moja kwa kuwa ni wewe umemuundia blog, basi ataweza kupata matokeo sawa na yako bila kufanya kitu na asipoyapata haha…

photo of women at the meeting
Photo by RF._.studio _ on Pexels.com

Na hela inaweza ikawepo ndio ila mtu afahamu basics kabisa amekuja tu kwa kukurupuka, so hata kama kazi itakunufaisha kwa muda huo. Inaweza kua damaging baadae, akati ni kitu ambacho kilikua kinakwepeka.

Na ukiamua tu kufanya kazi husika kwa kua una shida ya hela, nk. Basi hutoweza kuifanya kwa ubora maana hata wewe kichwani mwako utakua unajua hapa hata nikikesha naweka features hizi na hizi, huyu mtu hatozitumia ipasavyo. Hivyo hakikisha na wateja wako , wanaelewa ABC za kile unachowafanyia kwanza.

Kitu kingine kama malipo hayako sawa, au kuna kitu yeyote kweye namna unavyofanyaga kazi haijaenda inavyobidi kwenda then hutoweza kuifanya kazi husika kwa asilimia mia. Hivyo the end result kua damaging kwako na mteja.

Factor ziko nyingi na zinatofautiana na mtu na mtu. So wakati unapokea kazi, au kama ni freelancer na unachagua kazi za kuomba, basi chagua kazi ambazo utakua umejiridhisha kwenye angle zote unazohisi ni za muhimu na baad ya hapo, uzifanye kwa moyo mmoja and as good as you can.

Haijalishi ni kazi ya elf kumi au ya millioni. Naamini matokeo yatakua rewarding. So ku conclude kwa hapa, naweza sema be selective with the kind of jobs you pick/accept. Na ukishazikubali, zifanye ipasavyo.

Haha, au nieleeze tena kwanini? Anyways, twende kwa point inayofuata.

4. Try As Best As You Can To Honor Your End Of The Deal

Haha huku UpWork nimekuepo almost 5 Years now

Kuna wakati utatokea, kwenye kazi utakazochagua, (haha hii ilikua inanikuta sana UpWork) unakuta kazi ume i assess vizuri, umeridhia malipo, na client umeona ni mtu anajielewa na anajua anafanya nini, so unaizamia, giving it your whole.

Lakini bado inatokea mikengeuko ya hapa na pale. Whatever happens jitahidi uwezavyo to keep things professional and honor your end of the agreement.

Itatokea more than often, client mtapishana ukiwa kati kati ya kazi. Mnaweza kua mmezinguana kwa kazi hio hio au unakuta ni kitu kingine hakihusiani na kazi husika. Likitokea hili, haijalishi ni nini, as long as tayari ushaianza kazi husika, basi imalize.

Kama ni discount ulimpa mteja cause maybe of their best behavior haha afu ukaja kutana na mauza uza kati kati ya kazi haimaanishi discount sasa uitoe, iache iwepo kazi iishe. Mambo mengine yaendelee.

person signing paper
Photo by Cytonn Photography on Pexels.com

Hii wanaeza elewa graphics designers. Haha mtrja anaweza kuambia nataka Design yangu iwe ABC. Na ukamuuliza yaani iwe hivi kabisa akasema ndio.

Then unaiunda unampa design nzima anakuuliza mbona umeniwekea hii rangi ya kijivu wakati nlisema pink. Haha.

Then ukaeka pink. Akakwambia sijapenda inavyofanana. Em irudishe ilivyokua sema ongeza nyekundu. Ukiwa ni beginner unaweza sema hizi ni pigo gani? Ushauri wangu ni maliza kazi.

Baada ya kazi, kwendana na the whole experience basi unaweza kuamua if it’s wise kuendelea na kazi za aina hio au hamna.

Chochote kitakachotokea in-between kisiharibu au kufuta kitu chochote ulichokua umeji commit kabla ya kazi kuanza. Nadhani hapa sipaswi hata kuelezea kwanini. Itakusaidia sana kwenye kazi nyingi zijazo, if you’ll honor your word no matter what.

Na tukiwa kwenye swala hilo hilo la ‘honoring your words‘ twende kwenye point inayofuata;

5. Tilia Mkazo Neno ‘Uaminifu’

Virtual Cards : Ili Kuepuka Shida, Wakati wa kulipia mambo za Client mpya, basi huunda Virtual Card mpya maalumu kwa ajili ya malipo yeyote yatakayohusika na Project yake | Kainetics

Kila mtu ana mapungufu yake, ila ukiamua kufanya kazi yeyote ile mtandaoni, wewe pamoja na hayo mapungufu yako, jitahidi uwezavyo kua muaminifu.

Shida moja wapo itokanayo na mambo za kufanya issue yeyote online kibongo bongo, iwe ni wewe mwenye ujuzi, au mteja mwenyewe, kuanzia siku ya kwanza mtakayoanza kuongea…

Haijalishi nani kamtafuta nani. Haha, kila mmoja wenu atakua anahofia kutapeliwa.

Mteja akiwa ana interact na wewe kichwani mwake lazima kuwe na hofu ya asilimia kadhaa kua kuna probability yuko ana deal na tapeli.

The same ina apply kwa wafanya kazi wenyewe. Haha, wapo wateja ambao ni matapeli pia. Utapewa kazi utafanya utaituma for assessment, utakua blocked kabla ya malipo.

Hizi ni mambo ambazo zipo. So jitahidi from the get go, kwa kazi yeyote ile utakayoifanya, iwe ni ndogo au ni kubwa, uifanye kwa uaminifu. (Na uifanye kwa ubora wa asilimia mia kama nilivyokwisha sema huko juu)

Uaminifu ndio kitu pekee ambacho kitakusaidia kupiga hatua, ukiwa beginner, na hata huko mbeleni mambo yakianza kueleweka.

Uaminifu ni mtaji—Wahenga

Sijaunda tovuti nyingi kiivyo, ila nimeziunda za kutosha kufikia sasa. Kwa 2024 peke yake nadhani project za web design tu zina fika 150+ na hapo sikua deeply focused huko.

Niko naongea tu simple simple ila nakumbuka mwanzoni kabisa kipindi naanza kuunda websites kwa ajili ya watu wengine, nlikaa week saba hivi, kabla ya kupata mteja wangu wa kwanza. Haha huyu namkumbuka jina, na bado tunaongea hadi leo.

At the time, ujuzi nlikua nao ndio, ila sikua nimewahi kumuundia mtu yeyote tovuti, so sikua na portfolio, kila biashara/kampuni/taasisi nliyokua nawatumia ujumbe (email/DMs) kuwaambia nimeona hawana website, au website zao ziko na muonekano mbaya na niko vizuri kwenye sekta hio, so naomba kazi , walikua wengi wananikalia kimya.

Waliokua wakijibu walikuwa wananiambia naomba kazi zako tuone. Ukiwaambia hujawahi kuunda kabla, basi wanapotea.

data codes through eyeglasses
Photo by Kevin Ku on Pexels.com

And that makes sense, maana kwanini mtu akupe kazi wewe ambae hujulikani, na huna experience yeyote wakati unaweza kua tapeli? Na kwanini mtu achukue hio risk kwako wakati wapo watu huko wana majina tayari na washa establish msingi na walau portfolio zao ziko?

Sema sikuacha kutuma DMs na emails, kila ile hali ya kukata tamaa ilipokua inapungua. Until one day, siku moja naamka, nikakuta kuna shirika wamejibu email, tofuati kidogo na majibu nliyokua nimezoea kupata;

Hio siku nliulizwa uko sehemu gani? Na nadhani kwenye kujibu pale nliombwa namba nikapigiwa, nikaukizwa maswali na huyu bro, na japokua maswali niliyajibu vizuri bado alikua ana hofu ya kuwepo probability naweza kua tapeli, and that was understandable.

Mimi pia haha, nlikua nahofia nae asije kua tapeli. Maana enzi izo ili kupunguzia hao potential clients mashaka, nlikua willing kufanya kazi kwanza wanilipe baadae. Na wapo walioishia kuniblock nilipomaliza.

So nakumbuka sote tulikua tunategeana, lakini this guy decided kuniamini, na hivyo ndivyo nilivyopata customer wangu wa kwanza. Japo bei zilikua majanga haha.

Kazi nyingine zote zilizofuata kutoka kwa this brother na hilo shirika, sikupewa kwa kua I was the best Web Designer au sababu nyingine zozote za ziada (sikua na experience kiivo) ila nliendeleaa kupewa kazi nyingine na nyingine kwa kua nlipoaminiwa mara ya kwanza, sikuvunja uaminifu.

full frame shot of computer
Photo by Tranmautritam on Pexels.com

Najaribu kusema nini, kama unataka kujiairi online kwa kufanya kazi za watu wengine, basi fahamu ile tu kupewa kazi, ni mtu kaamua kujitoa ufahamu akijua ni either atapata kile unachoahidi au utageuka tapeli umblock. Lakini pamoja na kuyajua hayo, ameamua kubet, na kukuamini.

Usije chezea io. Maana kama beginner that’s the only way, utapata watu. Na ukiaminiwa ukaaminika, there’s a bigger chance zitafuata kazi nyingine, sometimes kubwa hata kuliko ile uliyofanya.

Pia Soma: Mambo Kumi Ya Kuzingatia Kama Kijana Ukiwa Kwenye Utafutaji

Simaanishi usiwe bora, hapo kwenye ubora hakikisha umejipika kisawa sawa and you’re good at what you do. Lakini huko kua vizuri hakutoshi, kama kuaminika ni shida. Kila mtu na mapungufu yake, ila jitahidi uwezavyo kwenye hili.

Sema bado, don’t over do your part. Ukiwa open with your process, ukawa transparent na bado mtu akawa na mashaka nawe, don’t sweat it. As long as you’re true to yourself, naamini watu sahihi watakupata kwa wakati ambao hata wao, watakili kua ni sahihi pia.

6. Ijue Thamani Yako & Know Your Why

So far, Blog ya Kainetics ina jumla ya Post 15 (+ hii)

Whatever it is you’ll be doing, as long as ni kitu utakua unafanya mtandaoni, then iko fair kusema every now and then utakutana na situations zitakazokuchanganya na kukupa confusion kuhusu thamani yako, in general.

Hakikisha hauwi confused. Na ukiwa confused, jikumbushe the root cause of your hustle.

Kuko na watu kibao ambao utakuta wanafanya kitu kile unachofanya tayari, wapo ambao wanataka waanze kukifanya…wapo ambao wameanza jana, so probability za kwamba wewe ni wa kwanza ziko finyu sana. Ila haimaanishi hii inabidi iku discourage.

Maana mambo yanayotusukuma kuhangaika, malengo tuliyonayo hayaezi kufanana. Wapo wanafanya whatever they are doing, for leisure, wapo wanafanya for money, wapo wanafanya for fame, wapo wanafanya for fun. Wapo wako na bajeti ndefu za kuchoma kufanya mambo yao yaende, na wapo hawana hata mia. Don’t get yourself confused.

Na nikisema usichanganywe. Namaanisha usichanganywe na hao hao watu, ila pia usichanganywe na clients ambao wame interact na watu wanao operate different na unavyo operate.

photo of dollar bills on a laptop
Photo by Photo By: Kaboompics.com on Pexels.com

Kama yupo Graphics Designer anafanya kazi yake kimasikhara, au anafanya kazi yake kwa njaa…then chances zipo kubwa hata pricing model yake itakua chini sana as long as apate chochote kitu, kwa situation aliyonayo inaweza isiwe mbaya.

Shida inakuja mteja ambaye amekua akifanya kazi na watu wa hivyo, kwa kua na we ndizo kazi unazofanya, anaweza taka kukuaminisha that’s your worth and that’s the price you should be taking. Don’t get yourself confused.

Pia inaweza tokea unakuta unafahamu kazi zako unazifanya kwa bei fulani na unajua unazifanya vizuri, ila bado kwa hio bei hupati wateja (haha hii inanitokeaga hata mimi) alafu unakuta kuna mtu mwingine, kazi zake ziko low quality sana , ila anapata watu, tena muda mwingine kwa bei kubwa kuliko hata zako.

Hii inaweza kukufanya muda mwingine ujihisi kuna kitu unakosea, au kuna namna unaji price vibaya, nk. Ila kama hujui wenzio wanaharibu shi ngapi kwenye matangazo, au wanajuana na kina nani, au wanafanya issue zao kiaje, don’t stress yourself or comprise your models.

Kwenye situation kama hizi jambo la muhimu la kujikumbusha ni kwanini bei zako ziko hivyo zilivyo na kwanini unafanya kazi kwa kufuata misingi io uliyojiwekea. And as long as you’re delivering na umezingatia mambo mengine yote muhimu, then you’re good to go.

7. Unda Passive Income Systems Kadhaa

Swali lilofanya niandae makala hii ya leo | Kainetics

Kwenye hii makala kuanzia huko juu nadhani nimekua nikishare screenshot baadhi baadhi za venture zangu nyingine nyingine ninazojishughulisha nacho ukiachana na mambo haya ambayo yako known kwenye hii blog kua ndio mambo ninayojishughulisha nayo.

Huko mwanzo kabisa, nimeshauri kua kati ya Kuchagua kitu kitakachojenga Awareness around jina lako au Kitu kinachokuingizia Hela, basi chagua kitu kinachokuingizia hela.

Ikibidi usiwe nacho kimoja. Kua navyo kadhaa. Hii itakusaidia kufanya mambo yako yaende hata kipindi ambapo hutokua na clients/projects mpya.

Maana ukiishi kwa kutegema clients kuna muda watakosa, na kama huna kazi nyingine utakua unafanya mbali na issue hizi za online, basi maisha yatakunyoosha (Naongea hivi from experience pia)

banknotes and calculator on table
Photo by Tima Miroshnichenko on Pexels.com

Ziko ninche kibao unazoweza kudeal nazo huko YouTube sio mpaka uanzishe channel inayokuhusu moja kwa moja. Au itakayokulazimu ku interact na audience/kuonesha sura au kuongea…na nani kasema ni lazima audience iwe ya Kiswahili?

Unda faceless channel yako, kwenye ninche uliyoifanyia research ya maana , komaa nayo hadi ianze kua Monetized na baado ya hapo automate the rest of the process iwe inakuingizia chochote kitu kila mwisho wa mwezi.

Na kama utaweza kua nayo channel moja ya hivii, nini kinakukataza kua nazo mbili au zaidi? (Haha usiniulize niko nazo ngapi)

Unaweza kua na blog uka idedictae kwa ajili ya Adsense tu, mambo ya kujulikana kua una ujuzi kwenye issue husika and etc ukaya sacrifice lakini bado blog husika itakuingizia chochote kitu, so it’s not a bad investment. Na ikishakua monetized una automate the rest of the proces ili ufocus na mambo yako mengine. Na ikbidi unatafuta tu team ya kuendeleza mambo za kuandaa content nk.

Na kama utaweza kua nayo moja, kwanini usiwe nazo mbili au zaidi?

Idea ziko nyingi. Point ni tafuta kitu inayoweza kukuingizia hela bila wewe kufocus nayo 100% na ukiweza kukifanya vizuri kikakupa matokeo, kwanini usiwe navyo kadhaa?

Unda Digital Products, fungua store yako ya Shopify uza huko. Kama utaweza kufanya na ukaanza kuona results, tafuta team or automate the rest of the process, na ikibidi kua nazo kadhaa.

Hizi njia zote nazo ongelea, hazitokupa jina, hakuna atakayekujua kupitia hizo, hazitokupa umaarufu wowote ule, ila maybe, just maybe, unaweza usilale njaa. Na kua flexible with the kind of projects unazofanya kwa urahisi zaidi, maana there will be other sources of income to help.

Hitimisho: Stay Humble & Usiache Kujifunza

Haha, mara moja moja hucheza haka kajitu kukiwa hakuna network. High Score yangu ni 5,218 hahaha

Who knows, maybe uko na njaa ya mafanikio kama mimi. Maybe unajituma uwezavyo, haudharau kazi, ndogo kwa kubwa, as long as unalipwa accordingly…

Maybe haufanyi kwa masikhara, unakesha ikibidi, huachi kujifunza, una adapt na muda na unajitahidi kuipa kila project unayofanya 100% zako…

Maybe umezingatia baadhi ya vitu nimeshauri, vingine umevitoa kwingine, vingine umevijiwekea mwenyewe na hatimae umeanza kuona matokeo…

Haha maybe ni izo passive income streams zako, au ni kazi unazopata zinalipa sasa, umeanza kupiga hatua (hatua ziko subjective… maybe umeanza kusanya assets, ni ununue ka usafiri, au ujenge kanyumba, au u upgrade pc yako, au uanze kua na savings zinazo eleweka…)

Whatever it will be , however your story will be; Stay Humble.

Sio uanze badili attiude haha, haijalishi ni kwa watu umewazidi au wamekuzidi, as long as they will be clients, haijalishi project ni kubwa, au ni ndogo, treat them with respect.

Kwenye hizii ma kazi unakuatana na all sorts of people…hakikisha kwa yeyote utayekutana nae, haijalishi situation imekua nzuri au mbaya, hakiksha huachi kujifunza/kufundishika.

breath word on a white card
Photo by Eva Bronzini on Pexels.com

Kuna muda clients watatumia hisia kuliko logic. Kuna muda utafanya hivyo wewe, kuna muda watakukwaza. Kuna muda utawakwaza pia, always self-assess. Na utakapoweza weka hisia zako pembeni.

Haha ninavyoongea sasa utadhani nani vile (hapa ilifaa niweke emoji ya kucheka) sema ndo huu ushauri wenyewe tunapeana.

Shukuru kwa chochote utakachopata, kiwe kidogo au kikubwa. Always be thankful.

Kwa kazi yeyote utakayofanya, do your best and hope you’ve done enough.

Usisahau kupumzika.

Consider kutafuta miwani inayo cancel bluelight mapema, utajishukuru mbeleni.

Huna laptop? Sio lazima sana. I do most of my stuff kwa simu, unless iwepo kitu ambayo ni ya lazima kufanya kwa laptop. So unaweza kuanza na simu yako, na ku grow pole pole.

Mambo yako prone kua magumu mwanzoni, jitahidi usi give up.

Sijui utakua unajihusisha na issue gani, whatever it is jitahidi kuhakikisha unaifanya vyema, na ifanye kwa akili.

Usifocus kiivo na mambo za kujulikana. Tafuta means zinazokuingizia hela kwanza na focus na hizo kwanza.

Usishidane. Ikikubidi kutafuta ushindani basi shidana na your previous self na focus kua bora kuliko ulivyokua jana.

Omba inapobidi. Na usifocus saana na hustle ukasahau ndugu na watu wako wa karibu.

Zingatia hayo yote, na mengine yajitafutie mwenyewe. And maybe…unaweza kujiita Digital Nomad.

I hope nimejibu maswali yote muhimu niliyokua naulizwa recently. Kama yapo zaidi, feel free to comment. Haha popote penye spelling errors, nisamehewe. Nadhani baadae nitarekebisha. That said, Good luck.


Discover more from Kainetics

Subscribe to get the latest posts sent to your email.