Network Marketing kwenye kizazi chetu cha kidigitali, sio neno geni sana. Haswa kama umeweza kufika chuo, basi kwa namna moja au nyingine, itakua ni kitu ambayo umewahi kusikia.

Hata kama hujafika chuo, bado naamini sio neno geni kwenye masikio yako, na kama ni geni. Basi kuna maneno kama LBL na FIC yanaweza kua sio mageni saaana maana kwa hivi karibuni yalitrend.

Kipindi hizo kampuni mbili zimeibuka ibuka, wapo watu tunaofahamia fahamiana kidogo walinicheck kuuliza kulikoni;

Izo network marketing ndio mambo gani?’

‘Tukaweke hela huku hivi, au ni matapeli?’

selective focus photography of filled bottles
Photo by Davide Baraldi on Pexels.com

Na maswali mengine kama hayo. Kama ulikua na maswali kuhusiana na izo mambo basi humu tutaziongelea kwa machache na kujibu baadhi ya hayo maswali muhimu; Network marketing ni nini? Ni utapeli au ni issue za halali? Na je unaweza kuingiza pesa kwa kufanya izo mambo au ndio unapigwa na kitu kizito?

Network Marketing Ni Nini?

close up photography of yellow green red and brown plastic cones on white lined surface
Photo by Pixabay on Pexels.com

Network marketing kwa kuifafanua kutumia Kiswahili kisicho rasmi, ni aina ya kujiingizia pesa mtandaoni na nje ya mtandao kwa kufanya marketing/masoko/matangazo inayofanywa na baadhi ya makampuni kwa kutegemea walengwa wake(clients/wateja) ndio wa promote bidhaa/huduma zao kwa ahadi za kamisheni kwa kila mtu mteja wao atafanikiwa kuleta. Au kama ilivyo kwenye jina lenyewe; ‘kumuongeza kwenye network’

Kampuni zinazofanya hizi mambo za Network Marketing, huwa business models mbili;

  • Moja, huwa na bidhaa au huduma ambayo inaweza kua physical au ya kidigitali isiyoshikika ambayo huitaji kununuliwa kwanza ndio uwe sehemu ya network yao.
  • Mbili, huwa na referral system ambapo ukishakua sehemu ya network, unapewa link unique au referral code ambayo utashauliwa kushare na ndugu na jamaa zako wa karibu, uwashawishi nao wanunue kitu ulichonunua ili uweze kupata kamisheni na kuingiza hela. Na wao ili waweze kuingiza hela itawabidi wafanye ivyo.

Hizo referral system zipo za aina nyingi; Zipo Binary, Uni Matrix systems na Matrix na system husika hu dictate ni namna gani watu utakao wa refer watakuingizia profit, kwa level ngapi na kwa kiasi gani.

Kama ushagasikia mambo za mguu wa kushoto na mguu wa kulia sjui na mguu gani haha, mambo zenyewe ndio hizi.

Sitaki kuongelea hayo mambo in deep kiivo ila unaeza beba keyword muhimu ukaenda kuzigoogle ili kufahamu kwa kina. Na kuendana na maelezo zilivyokaa sasa, haina budi kwenda kwenye swali la pili;

Je, Network Marketing Ni Utapeli?

close up shot of dollar bills
Photo by Tara Winstead on Pexels.com

Hapa jibu linategemea na kama unataka jibu refu, au jibu fupi. Jibu fupi ni; Ndio. Network Marketing in general ni utapeli.

Kama uliwahi kusikia kimsemo cha;

Ukiitwa kwenye fursa, jua fursa yenyewe ni wewe…

Sasa huku kwenye Network Marketing ndio kina apply kwa asilimia zote. Na nyingine kumi za nyongeza.

Ili aliyekualika apate hela, lazima wewe ulike hela kwanza. Na ili wewe upate hela, lazima utakaemualika alike hela. Na the same ina apply kwa huyo utakaemleta. Na siku watu wakiachia kuja, inamaanisha na mzunguko wa hela unaishia hapo. Maana hela ya mtu anayejiunga leo ndiyo hutumika kumlipa mtu wa jana.

a man in black sweater holding letter board with fraud text
Photo by Tima Miroshnichenko on Pexels.com

Kila kampuni inayofanya hizi mambo hujanna mbwembwe zake; hawa watakuambia, hela yako tunaiwekeza kwenye madini, wengine wtasema tunamiliki maduka hela yako tunawekeza huko, wengine ni mashamba, wengine watasema wanafanya Forex, wengine watasema wananunua stocks, ila haya yote hua ni kufunika kinachoendelea behind the scenes.

Ambacho ni nini? Well, hakuna kinachokua kinaendelea nyuma ya pazia haha. Ni uje, ulete hela, upewe link, utafute wengine walete hela. Wapewe link. That’s why, Network Marketing ni utapeli. Aina hii ya utapeli huitwa Ponzie/Pyramid Scheme. Kwendana na nature ya utapeli unavyofanyika.

Je, Unaweza Kuingiza Pesa Mtandaoni Kupitia Network Marketing?

bank notes
Photo by Suzy Hazelwood on Pexels.com

Jibu la hapa naweza kusema ndio na hapana. Inategemea na kichwa chako mwenyewe, na uwezo wako wa kusoma majira.

Jana ilikuwepo hio LBL waliotapeliwa ni wengi. Ni mamillioni ya pesa. Lakini upande wa pili, wapo walioingiza pesa kwenye mamillioni pia.

Kabla ya hio zilikuwepo nyingine. Na najua bado zitaibuka na nyingine, na bado watakuwepo watakaoingiza hela, na watakaotapeliwa. Hio ndo nature ya hizi ponzie schemes.

Unaingizaje sasa hela?

Kama ni mtu wa kujilipua, basi unaweza kuingiza hela kutumia haya ma network marketing kwa kuyawahi mwanzoni kabisa yakianza ku operate. Yaani unahakikisha uko kwenye ile batch ya mwanzo kabisa (week mbili/tatu za kwanza)

Kitu cha kuweka kichwani ni kuzingatia kua kuko na probability kubwa kua utakua una deal na matapeli. So, hela yeyote utakayoweka huko, iwe hela ambayo uko willing kupoteza.

low angle photography of structure
Photo by Miriam Espacio on Pexels.com

Kwa kua pyramid scheme zinavyofanya kazi, ni kwamba mtu wa jana analipwa na yule atakayekuja leo/kesho, ukiwa wa mwanzoni kabisa, basi uko na probability nzuri ya kuingiza vi hela kadhaa.

Kitu kingine cha kuweka kichwani, ni kua hizi huwa hazidumu. Na kudumu kwake kutataegemea na umaarufu wa platform husika. Ikijitahidi ikapita miezi mitatu ikiwa bado iko active, basi inaweza hold out hadi mwaka au saa nyingine miezi 6 tu, then mfumo unaharibika. So muda wowote tu unakaa kwa machale.

Je, Ni Kitu Ambayo Nakushauri Ufanye?

Hamna.

Ku engage na platform husika huku unajua ni matapeli, na ukaweka hela yako ni risk kubwa kidogo. Na sio risk ya lazima.

Zipo njia nyingine zisizo na maluwe luwe ambazo unaweza tumia kujiingizia kipato cha uhakika online na offline, kwa hela hio uliyonayo hivyo focus huko ikibidi. Ili kuepukana na mi pressure na msongamano wa mawazo usio wa lazima.

Maana kila mtu sio risk taker.

Hitimisho

an artist s illustration of artificial intelligence ai this image depicts how ai could adapt to an infinite amount of uses it was created by nidia dias as part of the visualising ai pr
Photo by Google DeepMind on Pexels.com

Kwa mafupi hio ndio network marketing. Hivyo ndivyo inavyofanya kazi, na hivyo ndivyo baadhi wanajipigia hela kutumia izo izo ma platofrm japokua zinakua za kitapeli, na hivyo hivyo ndivyo wengine wanatapeliwa.

Neno la muhimu kuondoka nalo kwa hapa hivi ni hio ya kwamba; “Ukiitwa kwenye fursa, basi fursa yenyewe ni wewe mwenyewe. Amka.”


Discover more from Kainetics

Subscribe to get the latest posts sent to your email.