Mtandao ni sehemu kubwa na pana sana, penye muingiliano wa watu wa kila aina. Kama kuna watu wema na wenye nia nzuri, iko safe ku-assume kua na watu wabaya wapo pia.
Kama sio mgeni kwenye hii mitandao, iwe ni Facebook, Twitter, Instagram, au kokote unako maliza muda wako mwingi; then chanches za wewe ku interact na tapeli ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri.
Na kutapeliwa mtandaoni haimaanishi labda hauna akili, au ni mshamba, au ni kwa kua hauko informed kuhusu kitu fulani basi ndio maana unaweza kutapeliwa. Hamna. The fact that una akili, na ni mjanja, na uko na basic knowledge kuhusu kitu fulani ni baadhi ya vitu vinavyoweza kukufanya utapeliwe.
Tena, kwa urahisi— kama nitakavyokuja kuelezea kwenye hii makala fupi na natumai kufikia mwisho utakua umeongeza kitu, na next time itakus ngumu kutapeliwa (iwe umewahi tapeliwa before—au hamna)
Katika makala hii nitaongelea huo utapeli naaongelea ni hupi, aina gani ya watu wanatapeliwa na namna gani unaweza kuepuka kuwa kundi hilo. Bila kupoteza muda; Tuanze.
Yaliyomo
Utapeli Wa Mtandaoni Ni Nini?

Well, kutapeliwa mtandaoni, kwa maelezo yasiyo rasmi, ni pale mtu anaporubuniwa kutoa taarifa muhimu, na ikibidi hela, kwa ahadi za kupata kitu bora zaidi iwe ni kwa punguzo, bure au promosheni (huku hiyo yote ikiwa ni uongo)
Kama nilivyosema hapo awali, matapeli wa mtandaoni wanakuja kwa rangi za kila aina; wapo utawalipa kukufanyia kitu fulani na hawatofanya, wapo watakuambia kuna kitu fulani unaweza kupata kwa bei ya punguzo baada ya kulipia, na hutokipata.
Wapo watakuambia kuna offer/promotion sehemu na kuna kiasi unabidi ulipie kuipata, na hutoipata. Utapeli upo wa aina kibao. Inaweza kua promises za kazi, na unabidi ulipie tu gharama za form/maombi, nk. Na bado hutoipata kazi husika.
Baadhi Ya Njia Zinazotumiwa na Matapeli Mtandaoni
Ziko nyingi. Na inategemea na matapeli wenyewe ni wa aina gani. Wapo wanao operate binafsi, na wapo ambao ni makundi/magenge wanafanya kazi kwa pamoja kuibia/kurubuni watu.
Baadhi ya Aina Za Utapeli Maarufu Online;
- Matapeli kutumia majina ya Mashirika/Makampuni makubwa kuibia watu — Hii ni ile unakuta mataepli wanatumia majina ambayo sio mageni masikioni mwa watu, na kujifanya wanatoa offer, kughushi meseji za miamala kuaminisha watu, na kuwaingiza mkenge kuchangia hela kadhaa ili wapate offer husika.
- Wizi Wa Account Kwenye Mitandao Ya Kijamii — Utapeli mwingine unaofanyika ni unaweza kua targerted na hackers, ukatumiwa link ambayo kwa kuifungua akaweza iba account yako. Na then kuitumia kurubuni watu wako wa karibu kumtumia hela (na wao kutuma wakiamini ni wewe)
- Huduma Za Uongo — Aina nyingine ya matapeli ni wale wanao promote huduma zisizokuwepo. Mfano vifurushi vya MB visivyo rasmi, huduma za kukuwezesha kudukua na kusoma SMS za mtu mwingine, kuuza odds za kubet, na huduma nyingine nyingi zisizo rasmi.
- Kutumia Majina Ya Watu Maarufu — Aina hii ni unakuta jina la mtu maarufu linatumika ku promote kitu cha uongo/kisichokuwepo. Picha zao, video saa nyingine hadi sauti zinaweza tumika kujaribu kukuaminisha mambo yasio kuwepo na njia nyingine nyingi.
- Miujiza / Huduma Za Kiroho — Aina nyingine ya utapeli ni unakuta wapo watu wanajitangaza kama waganga au makundi ya ajabu, wakiahidi huduma kama kurudisha mpenzi aliyepotea au kukuacha, mali na utajiri, na mambo mengine kama hayo.
Aina Gani Ya Watu Hutapeliwa Mtandaoni?

Mtu akiwa anakuhadithia alivyo tapeliwa, unaweza hisi ana upunguani kidogo haha, na hio kitu ni ngumu kuelewa inavyotokea hadi ikukute. Lakini sio mpaka ikukute ili uelewe na ikibidi kuepuka kabisa. Iwe ni kutapeliwa mtandaoni au nje ya mtandao.
Watu wengine waliotapeliwa hufikia hadi hatua ya kuamini kuna dawa walipewa au kupuliziwa za kuwapumbaza. Ila siamini hivyo. Ili kuelewa kwanini mtu anatapeliwa kirahisi, kwanza tunabidi tuelewe ni aina gani ya mtu huwa anatapeliwa. Maana sio kila mtu anakuaga targetted na matapeli. So, aina gani ya watu hutapeliwa kirahisi?
1. Watu Wenye Shida (Shida Kwelikweli)
Kitu ya kwanza inayomfanya mtu awe vulnerable kutapeliwa huwa ni shida. Na nikisema shida, sio shida ile ya kawaida. Maana kila mtu, hata awe nani lazima huwa na shida. Ila shida ninazo ongelea hapa hivi ni zile shida, zilizotuzidi uwezo. Shida zinazotulaza macho, zinazotupa mawazo na kutukosesha raha.
Pia Soma: Mambo Ya Kuepuka Ukiwa Desperate Sana Kupata Pesa
Na muda mwingi huwa shida ya kifedha. Unaweza kuta mtu ana madeni ya riba kubwa, muda wa marejesho umefika na hana kitu, maybe consequences ni kubwa pia ivo yuko kwenye hali ya ‘sijui nifanyeje kupata hii hela kwa haraka.’
Muda mwingine yanaweza yasiwe madeni, ila maybe unauguza, au kuna kitu tu kinahitaji hela, na sio kuhitaki hela tu, bali unaihitaji haraka iwezekanavyo. Na hela nyingi ndani ya muda mfupi. Ukiwa kwenye situation yeyote ya aina hii basi ni rahisi kutapeliwa. Yaani rahisi mno.
Maana kwenye kutafuta kwako kwa suluisho, lazima utajikuta umeingia kwenye sites au sehemu matapeli wanakovizia (na hata ukikutana na post zao izo zinazo promise iwe ni offer au hizo huge returns, na unaona hio mi ushaihidi ya mchongo, ni rahisi sana kuamini)
Na hata usipo amini, unakua unaiambia nafsi yako iamini, maana hunanamna yeyote iliyobaki.
2. Watu Wenye Tamaa
Hakuna mtu anaweza kukiri hii kitu, lakini moja ya factors zinazo play part kubwa kwenye kutapeliwa kwa mtu ni tamaa.
Na nikisema tamaa, naongelea ile mtu anaangalia kile atakachopata na kujali the fact that kitakua kikubwa kuliko kile atakachotoa hata kama njia za kukipata kitu husika zinatia mashaka.
Mfano; kwenye hali ya kawaida, ukiwa na akili zako timamu, unafahamu kabisa kwamba bei elekezi ya kifurushi cha internet cha shillingi elfu moja ni unapata MB 450+ . Sio zaidi au pungufu ya hapo.
Kitu pekee kinachoweza kuku convince kushawishika utakapokuta mtu online anakuahidi GB 15 kwa mwezi kwa shillingi elfu tano tu. Wakati unafahamu kabisa io elfu tano inakupa GB 2 hivi, ni tamaa.
Na ni tamaa ambayo ipo in a way that mtu anaangalia kile atakachopata, na sio kile anachotoa (na hio inamfanya ajitie upofu kutokufikiria kama ile namna kitu husika inapatikana inaleta maana)
Kitu pekee kinachoweza kumfanya mtu anunue Odds za kubet, zile Correct Score kwa shillingi laki mbili, ukiacha shida, utakuta muda mwingi ni kwa kua ameona zile ma screenshots zinazokua zinapostiwa na tapeli. Ivo ile hela anayotoa anaona si kitu kwendana na ile atayopata akishaweka huo mkeka na ukatiki.
Anasahau kuwa na maswali muhimu kichwani kama, huyu anaeniuzia hizi correct score ye anazitoa wapi? Kwanini aniuzie badala ya kueka dau apige hela peke yake kimya kimya?
Tamaa, ukiacha shida, ndio kitu inaweza kukufanya ushawishike kiurahisi.
3. Ujuaji / The Informed-Persona Complex
Kwa asilimia kubwa, mtu ambae hana elimu kubwa, au uelewa mpana kuhusu mambo, ni ngumu kutapeliwa, kwa kua huwa anafahamu hana info za kutosha kuhusu kitu chochote kipya atakachokutana nacho, hivo hutumia muda mwingi na udadisi wa hali ya juu kujaribu kukielewa. Na tapeli, huchoshwa na maswali haraka hivyo kuliko kujichosha kujaribu kumuelezea concept mpya, anaona ni heri amuacha atafute yule ambae anahisi ana uelewa na concept husika tayari.
On the other hand, yule ambae ni msomi,ni rahisi kutapeliwa maana kwa kua ni msomi, hujiaminisha anaelewa. Hata mambo ambayo hayaelewi. Na hata mambo zikiwa zinatia maswali, huogopa kuuliza au kutaka kuelezewa kwa kina ili value yake isishuke/asionekane kilaza.
Muda mwingine inaweza isiwe hivyo. Labda una uelewa kidogo kuhusu topic fulani, na kwa kua una uelewa kuhusu kitu fulani, mtu akiongelea mambo kutumia maneno kidogo ambayo uko familiar nayo, hata kama mengine mengi ni mageni una amua kuamini kirahisi kwa kua yale machache unayojua kayatumia.
Hii ndio naita ujuaji. Watu wengi ambao wako kwenye category hii ni wale ambao hutapeliwa na ma guru, na waalimu wa mtandaoni wanao promise high returns, matokeo na mambo mengine kibao ambayo hata hayapo au hawawezi yatimiza. Na utakuta wanalipisha gharama kubwa ku enroll kwenye izo masterclass/webinar/course zao kwa kutoa vitu ambavyo viko basic sana au freely available kwingine.
4. Watu Wanaopenda Shortcut
Aina hii ya watu ni wale wanaopenda kupeleka mambo haraka kwa kuskip hatua zinazofahamika ili mradi wapate kitu fulani kwa haraka.
Na kwa kua wanapenda mambo kwa shortcut, wako radhi kufanya kitu hataka kama sio halali, au sahihi, ili mradi wafikie matokeo wanayotaka, and by doing so unakuta wanatapeliwa.
Unakuta mtu amechukua simu ya mkopo, anafahamu kabisa—kutokana na makubaliano baina yake na kampuni iliyompea simu—anabidi alipe shingapi, ila unakuta atataka kutafuta watu wanaoweza kuondoa ile program inayofunga simu asipo lipa (ili aitumie bila kulipa)
Mwingine unakuta anajua kabisa kama ana duku duku, au kitu ina mkwaza, au ana wasiwasi au ina mtatiza kwenye mahusiano yake, basi unabidi amfuate mwenza wake na kuliaddress tatizo.
Ila japo kua anafahamu, hivo, bado atatafuta njia mbadala za shortcut za kufuatilia mambo za mwenzie kwa njia mbadala (hawa ndio unakuta watatafuta watu wa kuwasaidia kusoma sms za wenzio au hata kutrack location) na kwa kua wako ivo ni rahisi kutapeliwa.
Mifano ni mingi. Unakuta unafahamu kabisa process za kuomba kazi, ajira zinavyotangazwa, mchakato mzima mpaka mtu ana ajiriwa zinavokua…ila bad anashawishika kutuma hela ya maombi kisa kaona kampuni fulani wana ajiri.
Kwa kua anapenda shortcut, hatotaka kufuatilia hata kwenye page rasmi za kampuni/mtu/shirika husika aone kama kitu alichoona ni kweli.
Unakuta anafahamu ofisi zao ziliko ila hatowezataka kufika au hata kuuliza kama kweli wana ajiri au wanatoa huduma au offer fulani. Huamini kwa kuchukua shortcut ndio wameweza kumbe ndio wamewezwa vizuri.
Mwingine utakuta anafahamu kabisa ili kuingiza hela, lazima uitolee jasho. Either ufanye kazi, au uuze kitu. Kanuni ya kuingiza hela ikogo simple ivyo. Ila bado utakuta mtu anashawishika kutoa hela kuwekeza kwenye mambo ambazo hazileti maana kisa kaahidiwa atapokea hela kubwa na bila kufamya chochote.
Mtu wa design hii atatapeliwa mpaka akili zimkae sawa.
5. Mbumbumbu
Aina hii ya watu wanaotapeliwa, ni wale wenye sifa zote hizo tajwa hapo juu. Unamkuta mtu ana shida imekaba kweli, au unakuta tu hana shida ni ugumu wa maisha mambo hayaendi vizuri.
Then, unakuta mtu huyo huyo bado ana mitamaa tamaa ya ajabu ajabu. Tena mtu huyo huyo anajikuta mjuaji na msomi, na anapenda shortcut.
Mtu wa aina hii namuita ‘mbumbumbu’ na anatia huruma, maana ni ngumu kumsaidia. Nakukmba usiwe mbumbumbu.
6. Bahati Mbaya / Targetted Victims
Sasa izo sifa nlizotaja so far sio nzuri kiivo. Ila haimaanishi kila mtu anae tapeliewa basi ana tamaa, au anapenda shortcut, au ana shida saaana.
Hamna. Unaweza usiwe na hivyo vyote lakini bado ukatapeliwa. Inawezekanaje? Well, inategemea na aina ya utapeli unaofanyika.
Wapo matapeli ambao hutarget wazee, na kuwadanganya danganya kujikuta customer support, either wa bank au mitandao ya simu na kuwapa maelekezo yanayoeza wafanya waibiwe salio zao kwenye simu.
Wapo wale wanatuma ma meseji ya ‘Ile pesa tuma kwenye namba hii’ hao ni ngumu kukutapeli. Ila inaweza tokea probability uko na mtu unasuniri akutumie namba umuewekee hela ikaingia meseji ya ivo na ukamtumia. Ukatapeliwa. Inakuaga circumstancial.
Muda mwingine unaweza tapeliwa kwa kua tapeli alipitia kwa mtu wako wa karibu, either ame hack account zake ivo ukahisi unawasiliana na yeye. Au amemtapeli yeye na kupitia yeye akakutapeli na wewe pia.
Utapeli upo wa aina nyingi ivyo unaweza kua victim tu wa mtu mjanja na mwenye utapeli uliotumia akili kubwa, hata kama na wewe una akili.
Hivyo, Uzingatie Nini Kuepuka Kutapeliwa Mtandaoni?

Kama umekua unasoma kwa umakini, nimesema sababu zinazoweza fanya mtu atapeliwe ziko nyingi. Ila chache kuu ni hizo. So kama hutaki kutapeliwa mtandaoni hakikisha unafanya na unakua na sifa tofauti na izo nlizotaja hapo juu, huku ukiongeza sifa ya ziada; udadisi.
1. Usiruhusu Shida Zikuendeshe
Je, uko na shida kubwa imekuzidi uwezo? Na ni shida ya muhimu. Acha kutumia hisia, usipanick. Jikataze kufanya kitu chochote ambacho usingejihusisha nacho kama io shida ungekua huna.
Mtu anae bet kila siku ni ngumu kutapeliwa na watu wanaouza correct scores maana anaelewa betting nqi bahati nasibu na kuna mambo mengi hutokea uwanjani ndani ya hizo dakika 90 hadi aibuke mshindi. So mtu kua na matokeo kabla hta ya mechi kuanza iko close to impossible.
Ila mtu ambae hajawahi kubeti ni rahisi kushawishika na hizi watu, kwa kua hajui na kwa kua ana shida basi anaruhusu shida imuendeshe.
That said; usiruhusu shida ikuendeshe. Au hisia. Iwe ni woga, hofu, sonona au whatever utakua una feel. Hakikisha hisia zako haziku control, na hivo kutofanya maamuzi yasiyoleta maana.
2. Punguza Tamaa
Falsafa ya kuingiza hela iwe ni mtandaomi au nje ya mtandaoni, ni either unauza kitu ndipo unapata hela, au unafanya kitu/kazi ndipo unapata hela.
Hivyo kitu chochote/mtu/kampuni/sijui na nini gani itakayokuja na kukuahidi kuingiza pesa ndefu, au fupi, au whatever—bila kufanya kazi yeyote ile ya maana, kimbia!
Hakunaga hela za hivyo.
Muda mwingi ukiona mtu anatumia nguvu kubwa kukupa fursa/kukualika kwenye fursa fulani. Most of the time fursa ni wewe mwenyewe.
Kama unafahamu bei ya kifurushi cha mwezi ni elf 20 mtu aje kukuuzia kwa elf kumi nawe ukubali, basi ukitapeliwa unastahili.
Unafahamu kitu x Dukani kinauzwa kiasi fulani. Mtu anakuja kukuuzia kitu kile kile kwa bei tofuati kabisa na unayofahamu, na huna namna ya ku prove kua huyo mtu yuko associated na bidhaa/huduma husika; shtuka.
3. Acha Kupenda Shortcut
Kubali kuenyeka na kuamini process ndefu, kuliko mambo ya kupata matokeo makubwa ndani ya muda mfupi. Kama unafahamu kua kitu fulani kina leta matokeo x ndani ya mwaka, mtu akija akakuahidi the same results ndani ya week mbili na wewe ukakubali, basi unakua umeyataka mwenyewe.
Acha kupenda Shortcut, na kona kona zisizo za msingi.
4. Kua Mdadisi (Acha Ujuaji)
Unaweza usiwe na tamaa, usiendeshwe na hisia, usiwe mtu wa kupenda shortcut, lakini ukatapeliwa kwa kua sio mdadisi, au huulizi maswali ya kutosha.
Kila concept utakayokuta nayo online, iwe una uelewa nayo, au ndio mara ya kwanza unaisikia, hakikisha haukubali kutoa hela yako mfukoni, hadi umeuliza maswali yote muhimu na ya msingi.
Na hadi pale utakapo kua umejiridhisha pekua zaidi.
Mtu anakutafuta anakuambia ‘Oi umesikia kuhusu Offer ya UNICEF Foundation’
Unakimbilia kuuliza ikoje hio?
Anakwambia ‘kuna hela kidogo unatoa wanakupa kama million mbili hivi.’ Na anakuonesha screenshot za miamala.
Badala ya kuuliza maswali zaidi unakimbilia kutoa hela kisa unawaza io hela utakayopata. Rafiki, utatapeliwa hadi akili zikukae sawa.
Na nikisema kuuliza maswali, simaanishi uulize muhusika tu. Maswali mengine unajiuliza mwenyewe.
Mfano, kwa haraka haraka, jiulize, kitu gani kinaweza fanya shirika likupe tu hela bila sababu yeyote?
Kwanini hakuna sehemu umesikia hizo mambo before. Na unajua wanatangazaga hadi kwenye TV na Radio?
Hivi ni kweli wanaitwa UNICEF Foundation?
Hio namba ninakotuma hio hela kwanini haina majina ya kampuni/shirika husika?
Maswali unayojiuliza wewe yatakusevu kwenye situation yeyote. Usikurupikie mambo.
Hitimisho

Nilipokua mdogo, nliwahi kufundishwa kua kabla sijavuka barabara, niangalie kushoto na kulia, nihakikishe hakuna chombo chochote cha usafiri kwanza ndio nivuke.
Hio ndiyo kitu nayoweza kukushauri pia. Wapo watu wanagongwa kwa kua wanaona kusurvey barabara kabla ya kuvuka ni ushamba, ni ka kitu kadogo ila unaweza kua surprised kufahamu idadi ya watu ambao wamegongwa kisa ka sababu kadogo kama hako.
Ni heri uonekane mshamba kwa muda, kuliko uonekane mjanja afu ufe. Haha. So, uliza maswali, ukikutana na mambo hazileti maana.
Sikiliza moyo wako, kama issue iko imekaa haieleweki, ukianza tu kuitilia mashaka achana nayo. Acha tamaa. Acha kupenda shortcut. Hata uwe na shida ya aje, usikubali kufanya mambo ya ovyo, au kutafuta hela za haraka haraka utatue. Hela haziji ivo.
Kumbuka unabidi uuze either kitu au huduma ndio upate hela, so ukikutana na kitu kina kupromise otherwise, weka alama za kuuliza za kutosha .
Hapo mwanzo nimesema mtandaoni kuna kila aina ya watu. Sio kila mtu utakae kutana nae mtandaoni ni tapeli.
Sema jihakikishie kwanza Ikibidi. Na usitake huduma zozote illegal na zisizo halali. Maana utatapeliwa na bado huna utakachomfanya aliyokutapeli maana huna pa kumshtaki, kuendaba na huduma uliyokua unataka.
Em nambie umemlipa mtu laki akupe app ya kuona sms za mtu, ale hela akublock, utamfanya nini? Au mtu akuahidi anafungua simu z mkopo kwa elf hamsini, utume na asiifungue utamfanya nini? Utampeleka wapi? Maana na wewe unakua unataka kuwatapeli waliokupa simu husika
So acha hizo mambo. Kua mdadisi. Kua attentive muda wote. Na ikitoeka ukatapeliwa, itakua kwa bahati mbaya tu and circumstancial and not otherwsie.
Discover more from Kainetics
Subscribe to get the latest posts sent to your email.