Huduma Zangu

Kama unahitaji kitu chenye ubora na kilichoundwa na Professional kwenye field husika, basi unaweza consider kufanya kazi na mimi na sitokuangisha. Huduma zangu zote nimeziorodhesha kama ifuatavyo;
** Pia Taratibu za kufanya kazi nimezioredhesha mwishoni kabisa hivyo usisite kuzipitia pia.
Web Design

Iwe unahitaji tovuti ya Kampuni, ya Biashara, Binafsi au Blog. Unaweza kunicheck. Haijalishi uko na bajeti ndogo, ya wastani au unataka kila kitu kiwe full package. Tovuti ninazo unda ni za kisasa, muonekano unavutia na ziko very responsive haijalishi zitakua accesed kwa Laptop, Simu au Tablet.
Huduma ya Web Design inakuja katika Package Tatu Tofauti; ENTRY LEVEL, PROFESSIONAL & EXTENSIVE.
ENTRY LEVEL
Hii ni kwa wale wenye bajeti ndogo mno, lakini wanahitaji kua na tovuti. Bajeti inaweza isiwe chagamoto kiivo, labda ni Beginner ivo hauhitaji tovuti husika iwe na mambo mengi kiivo ila iwe na mambo ya msingi na imekamilika.
Hii ni maalumu kwa wale ambao wako interested na blogging na wanataka waanze safari yao ya kujiingizia kipato online na kwa wale wanaotaka kufanya Blogging kama Hobby.
Mambo ya Muhimu kama Logo + Domain + SSL + Hosting Ya Miezi Miwili yana ambatana na hii Package.
Unaweza gusa button hapo chini kama uko interested na hii Package, nayo itakupeleka moja kwa moja WhatsApp ili tufanye kazi.
** Features nyingine unaweza ongeza mdogo mdogo kadri uanvyozidi kukua na Blog yako
PROFESSIONAL BLOG/ WEBSITE
Hii ni kama unahitaji tovuti iliyokamilika kwa iwe ni kwa ajiri ya biashara yako, au ni tovuti binafsi ya Portfolio, au kama unataka kufanya Blog professionally zaidi na iwe ina feature za kutosha kuhakikisha unaanza safari yako kwa umakini zaidi basi unaweza kuchukua Package hii.
Package ina ambatana na Basic SEO & Branding ili kusaidia kuonekana kwenye search Engines, Premium Plugins 10 + muonekano uliotulia.
Domain + Logo + SSL + Hosting Miezi 6 + Professional Email Address + Free Tech Support kwa Miezi 3 vina ambatana na hii Package.
** Bei ina range kuendana na idadi ya features utakazo taka.
EXTENSIVE WEBSITE
Kama unahitaji kuunda tovuti yenye features za Ziada, au Unique (iwe ni E-Commerce Store, Business Directory, Forum, Podcasting Website, au Subscription Based Website/Membership only) au idea yoyote uliyonayo wewe basi hii ndio Package ya kuconsider.
Iwe idea yako inahitaji kuundwa kwa PHP, Javascript, Boostrap, Laravel au Python, HTML5, nk. Tuwasiliane.
Website Optimization

Kama uko na tovuti tayari, lakini haina muonekano uliotulia, ina load kwa kuchelewa, inazorota au unataka kuiandaa kwa ajili ya kuiunga na Adsense kwa baadae hivyo unataka ifanyiwe marekebisho ya kawaida kama; kuibadili muonekano iwe ya Kisasa na Professional, ku optimize loading speed, na kuipangilia iendane na color palette ya Brand yako yaani kiufupi kuhakikisha inakaa sawa basi huduma yenyewe ndio hii.
Nayo ipo kwa Package mbili;
WO1 – Kwa ajili ya kurekebisha yale yote ya mhimu (kubadili template, ku optimize loading speed na muonekano mzima wa Blog, Color Palettes na Responsiveness)
WO2 – Mambo yote yaliyokwenye hio WO1 pamoja na mambo za kufix Schema, Sitemap ya tovuti, kufix duplicates, kueka Carnonical links na mengine yote ya muhimu.
** Huduma hii natoa kwa tovuti zinazotumia CMS ya WordPress na Blogger tu.
Website Improvement Analysis

Huduma hii ni bure. Kama uko na tovuti/website/blog na ungependa niipitie na nikupe recommendations ya mambo unayobidi kurekebisha au kuweka sawa ili tovuti yako iweze kufanya kazi na kuperform vizuri zaidi kwenye search engines. Basi usisite kunicheck na kunipa link ya tovuti yako niipitie!
SEO

SEO—Search Engine Optimization ni moja ya vitu vya msingi unavyobidi kufanya kwenye blog /tovuti yako ili iweze kuonekana vizuri kwenye search Engines kama Google na Bing mtu aki search.
So unaweza kua na blog, lakini bila correct Optimization usitokee kwenye Search Results na hapo ndipo inapokuja huduma hii.
Yenyewe, inapatikana katika Package tatu tofauti; Basic SEO, Technical SEO & Extensive SEO.
** Ikiwa mimi ndiye nliyokuundia tovuti/blog yako basi Basic SEO ni bure kwa Professional & Extensive Package which means utakua una appear kwenye Search Results from Day One.
Kama sijakuundia mimi tovuti na unataka kufanyiwa hii Basic SEO (On-Page Optimization, Caching, Lazy Loading Images na Google Integration), au hio Technical SEO (Off-Page SEO, Liquidity, Backlinks, AMP, CDN+more) au hio Extensive SEO (kama ni Shirika/Kampuni) basi unaweza wasiliana nami;
Bei zina range kuanzia TSH85,000/- (Basic SEO) hadi TSH215,000/- ~ TSH555,000/-(Technical SEO) na Extensive SEO ita depend na Scope nzima ya Project.
Social Media Branding

Kama ni mtu binafsi na una offer huduma zako online, iwe ni Instagram, Facebook, Tiktok (au kwenye mitandao yote kwa pamoja. Au unamiliki Online Media, au uko kwenye utaratibu wa kuanzisha na ungependa kufanya Social Media Branding, ili account zako ziweze kukaa Professional, Organized na baadhi ya vitu kwenye Workflow yako kua Automated, basi tunaweza kuwasiliana.
Bei zina range kuanzia as low as TSH65,000/– hivyo usisite kunicheck.
Premium Consultation

Ukiwa na dukuduku, maswali au unahitaji ufafanuzi kuhusu tipic fulani, usisite kuniuliza swali kwa muda wowote ule na ni bure. Ila kama unataka niweze kua part of your team na kuweza kuelekezana taritibu kadri project yako inavyo kua, iwe ni Podcast, Blog, Online Media au ni unahitaji Consultation based on Digital Marketing (unataka kua una run matangazo ku promote bidhaa/huduma au biashara yako online. Basi feel free kunicheck.
Consultation inaweza kua Monthly, au kwa Muda Mrefu; Miezi miwili na kuendelea. Kikubwa uweze kuona matokeo yale unayoyataka.
Huduma Nyinginezo

Kama nilivyo sema hapo mwanzoni humu naandika kuhusu mambo ambayo niko na experience nayo, hivyo huduma unayotaka iwe nimeorodhesha kwenye hii list, au lah lakini ni kitu nimeongelea na ni kitu unahitaji Iwe inahusiana na mambo ya Graphics, Video, Programming, Ads, Branding, nk.
Taratibu Za Kufanya Kazi Pamoja
Kufanya kazi pamoja ni simple na hakuna complications nyingi. Ninathamini Uwazi, Muda na Ubora wa Kazi husika. Hivyo ukigusa kitufe cha Kuwasiliana Nami na kuja WhatsApp basi inakua kufanya kazi na mtu anaethamini mambi yote hayo matatu, ikiwemo uaminifu.
Project zinafanywa katika hatua kuu nne muhimu;
1. Mawasiliano Ya Awali
Hii ni pale unapogusa kitufe kikakuleta moja kwa moja WhatsApp. Kwenye hatua hii tunaongea mambo ya muhimu ikiwemo kufahamiana kwa ufupi, kujua ni aina gani ya huduma unahitaji, na baadhi ya mambo nitakayohitaji kufahamu na kukufahamisha kuhusu project nitakuuliza/na kukujuza (ikiwemo project itafanyika macimum kwa ndani ya muda gani). Pia yakiwepo maswali upande wako unaweza kuuliza pia.
2. Malipo ya Awali (45%)
Baada ya kufahamu mambo unayohitaji yawe kwenye project/kazi husika nitakupatia namba ya malipo/Lipa Number, na utatanguliza asilimia arobaini na tano ya gharama za kazi husika na kisha kazi itaanza rasmi.
Wakati wote wa kufanya kazi utakua na access ya kuona kinachoendelea na the whole progress.
Ikiwa kuna taarifa zozote zinazohitajika, mapendekezo na kadhalika tutajuzana hadi kazi itapofika 80% kukamilika.
3. Malipo Yaliyobakia (55%)
Baada ya kazi kukamilika kwa asilimia themanini, ndipo utapitia na ku recommend maboresho ya mwisho, mapendekezo na mambo mengine kama hayo.
Baada ya kufanya hivyo, utafanya malipo ya kiasi kilichobaki, nami nitafanyia kazi mapendekezo yako na kukamilisha project nzima.
4. Makabidhiano
Baada ya kukamilisha project husika. Nitakukabidhi Login Details, na Data nyingine zozote mhimu (related to the project) na inapobidi utabadilisha password zako, na kuendelea na kazi zako.
Pale utakapokutana na changamoto yeyote, au kua na maswali, kama nlivyokwisha sema huko mwanzoni—ni bure so feel free muda wowote ule kuuliza.
The whole point ya kuwepo kwa Kainetics ni kua resource ya uhakika unakoweza pata Content zilizoshiba na zinazoongelea mambo husika kwa kina na katika lugha rafiki ya Kiswahili ili iweze kua kama reference point kwa mtu anayejifunza/ongeza ujuzi na kadhalika.
Hivyo tegemea falsafa io io ya mambo kua na uwazi, kwa kina na ubora hata kwenye kazi.
Wako, Frank Kai. Karibu.