Habari, natumaini sote tu wazima. It’s been a minute toka niandike post mpya humu kwenye blog. Mambo ya hapa na pale yalikua mengi, but hopefully nitakua naandika mara kwa mara kidogo.
That said; kwenye hii makala fupi ya leo, ningependa kuongelea hii kitu ya swali muhimu; ‘Kwanini?’
…na kwanini inabidi ulijiulize kabla ya kufanya maamuzi yeyote muhimu maishani mwako bila kusahau kwanini ni muhimu kutolisahau jibu lake baada ya kuamua.
Utangulizi

Kuna kauli moja nayoweza sema iko imprinted kwenye ubongo ambayo nimekutana nayo kwenye medium tofauti kanakwamba sikumbuki mara ya kwanza kabisa naisikia/nakutana nayo ikanikaa kichwani ilikua lini. Ila kauli yenyewe naikumbuka;
“Maamuzi yako leo, ni matokeo ya kesho.“
Kwa urefu, imekaa hivi;
“Maamuzi yako leo, ni matokeo ya kesho. Maisha unayoishi, na leo yako ilivyo leo, yanatokana na mamillioni ya maamuzi yaliyofanyika huko nyuma. Amua vyema, upate mema.“
Ni either iko ivyo exactly, au imekaribiana na kitu kama icho. Point ni kwamba inaongelea umuhimu wa ‘maamuzi.’ Kua maamuzi yeyote yale, yawe makubwa au madogo, yawe mazuri au mabaya, yawe ya kwetu au ya watu wengine, kwa namna moja au nyingine; yana determine kesho yetu inavyokua.

Hakuna mtu anayeijua kesho, ila uko na chances za ku guarantee kesho njema na yenye unafuu/hauweni kuliko leo kutokana na maamuzi utakayoamua kuchukua. Na hii haizungumzii maamuzi ya kibiashara pekee, au ya kimahusiano, kirohoo, nk. Ni maamuzi yote kiujumla.
Hata yale maamuzi yanayoonekana hayako significant; mfano nguo utakayoamua kuvaa, maneno utakayoamua kuongea, njia utakayoamua kupita, chakula utakachoamua kula,muda utakaoamua kuamka/kusinzia, kisomo utakachoamua kubase nacho, na mengine mengi ambayo yanaweza yasionekana yana umuhimu kwa wakati huo; hata yale mambo madogo kabisa, yako na uwezo wa kubadili muelekeo mzima wa maisha yetu tusipochagua vizuri.

Hii kauli imenikaa kichwani, kwa kua iko na ukweli wa kutosha (speaking from experience) ila sababu nyingine nadhani itakua ni kwa kua, japokua bado ni mdogo mdogo kiumri, yapo maamuzi kadhaa nliyofanya na mengine kufanywa na watu wengine wa karibu ambayo yamebadili mwelekeo mzima wa maisha yangu tena na tena. Baadhi yakiwa ni maamuzi mazuri, na mengine yakiwa mabaya. Na mengine yakiwa mabovu kupindukia.
Story Fupi

Haha, huko juu nimesema kiumri bado niko mdogo, japo personally nafahamu nimeshakua na kupevuka kifikra vya kutosha. Kuna baadhi ya maisha watu wanaishi, unakuta hawana budi kua watu wazima, wakiwa bado ni watoto.
Kwanini naongelea umri? Well, more often than usual, kwa wale watu ambao tumefahamiana online, hatujawahi kuonana kabla, na hatujuani kwa sura; hua wanakua na ka confusion kidogo wakiniona.
Utaskia ;
‘…kumbe bado mdogo…‘ ,
‘…kuna miaka nlikua na kuimagine utakua nayo, sikutegemea ndo utakua mdogo zaidi…‘
‘…kwa hii miaka yako,na vitu uanvyofanya haviendani haha…’
Na kauli nyingine kama izo. More often than usual, mtu akitaka kupunguza confusion aliyonayo, atataka afahamu kwanini? Like what’s your story, na kwanini unafanya izo mambo zote unazofanya? Mwngine atataka ajue, unafanyaga nini, specifically?
Ni muda kidogo umepita toka niulizwe hilo swali, ila nilipoulizwa leo mambo haya yote yakanirudia kichwani, na ndio sababu naandika hii post, ila kwanza nlikua naongelea maamuzi.
Mimi na Maamuzi. Maamuzi na Mimi

Kwa hii hii miaka yangu, kama ambavyo nimekwisha sema; Yapo maamuzi mazuri nimefanya na wamefanya watu, wengine wakiwa watu nisiowajua yakabadili mwenendo wa maisha yangu kabisa, tena na tena (in a good way)
Na kwa hii hii miaka, yapo maamuzi ambayo nimefanya, na yapo ambayo yamefanywa na watu wengine na yakaniharibia mambo mengi mno, haya for some reason yako mengi kuliko hayo mazuri.
Haha, kuna muda nikikaa nikajitafakari, aina ya maisha nimeishi, mambo niliyoona, kuanzia mwanzo huko hadi saa hivi, nakua nacheka mwenyewe. Ila sio kwamba kila kitu ambacho nimekutana nacho kinachekesha.

Mengine ni mambo mabovu kabisa hayaelezeki, mengine tumemwachia Mungu, na mengine tumeamua kusahau, mengine yametufanya tufute baadhi ya watu, na kwa mengine yamefanya nijiahidi kua nitajirekebisha na kua version bora zaidi ya nlivyokua jana. Haya ni kwa maamuzi mabovu ambayo nimeyafanya mwenyewe.
Kuhusu Maamuzi Yenyewe

Sio kila kitu utakachoamua kikakuingiza kwenye majanga, basi uliamua vibaya. Hamna. Muda mwingine, mambo uliyoamua kufanya, kwa nia njema yanaweza yaka backfire kisa tu sababu nyingine ambazo hata hazihusiani na wewe moja kwa moja, (watu watakugeuka, timing inaweza isiwe sahihi, bahati mbaya, nk) lakini pia zipo situation ambazo sababu itakua wewe mwenyewe, ukatae au ukubali.
Maybe ipo siku nitaandika kuhusu baadhi ya majanga ambayo nimekutana nayo kwenye hii miaka yangu mingapi nliyonayo.
Upande wa pili, Yapo maamuzi mabovu ambayo yatafanywa na watu wengine, muda mwingine utakuta ni watu ambao huwajui kabisa, lakini yataku affect moja kwa moja bila kujua;
Mfano; kipindi cha Corona/Covid-19, kuna watu walikua wanajua wako na dalili zote za huo ugonjwa, lakini bado walikua wanaingia sehemu zenye michanganyiko mikubwa ya watu, hivyo kupelekea watu wengine kua infected.

Utakuta yupo mtu alikua anafuata safety protocol zote. Kajifunika, kanawa mikono as often as possible, ako na barakoa lakini bado akapata covid kwa kua mtu mwingine alikua careless.
Kwenye hizi interviews, unaweza kua na vigezo vyote na sometimes hata kua overqualified lakini bado ukakosa kazi kimasikhara kwa kua mtu tu huko alipenda jina la mtu mwingine linavyo sound, kuliko la kwako.
Wazazi kwa sababu wanazojua wao wanaeza kuamua kuachana bila kufikiria ni namna gani ita affect ukuaji wa watoto wao. Na decision moja simple kama hio, ambayo inaweza isiwa-affect wao moja kwa moja, inaweza badili mwelekeo mzima wa maisha ya watoto wao, milele.
Hivyo, maamuzi ya watu wengine yanaweza kutu affect, directly na indirectly pia. Ila kwa hapa hivi nitaongelea maamuzi binafsi.
Maamuzi Yangu Mabovu

Ingekua ni summarize kisababishi cha matatizo/majanga yote makubwa ambayo yamenikuta, na ambayo yamenikuta kutokana na maamuzi niliyofanya mwenyewe; basi sababu zote zinaweza kua summarized kua hayo mambo makuu matatu;
- Kushindwa kusema hapana
- Kutojiweka nafasi ya kwanza, inapobidi
- People-Pleasing
KUSHINDWA KUSEMA HAPANA
Naweza sema to some-extent, niko self-aware. Hivyo kuna muda hata ukiwa pll maamuzi ambayo unaona sio sahihi, au yatakuumiza baadae, unakua unajua kabisa. Lakini bado unayachukua ivo ivo. Na mwishi wa siku unajikuta umebaki tu kua mtu mwenye hatia. Kwa kua kwa baadhi ya vitu utakua unajua ‘hapa niko najikosea kabisa…’

Sijajua kisababishi kikuu hadi mtu anakua anakutana na ugumu wa kusema hapana na kujisimamia inapobidi ni nini. Ila hii ni kitu ambayo kwa muda, kwenye kukua kwangu imekua ikinisumbua. Na ukishajijengea ka reputation kua ‘fulani hata umwambie nini hakatai…‘ basi jiandae kujikuta kwenye situation mbovu mbovu za kila aina.
Zamani huko nlikua najiambia labda ni nafsi ya mtu ndi inakua hivyo, kua binadamu tunatofautiana, so maybe, niko na roho nzuri imezidi ndio maana (haha hiii inanichekesha hapa ninavyoiandika) ila sidhani kama kisababishi ni icho. Na bado sijui vizuri kwanini ilikua hivyo ilivyokua.
Ninachojua ni kwamba, kwa namna moja au nyingine, iko inahusiana na izo sababu nyingine mbili, haswa hio ya kutojiweka mstari wa mbele.
KUTOJIWEKA NAFASI YA KWANZA, INAPOBIDI

Nayo hii, kwendana na namna tumelelewa au sijui niseme ni namna nilivyokua; nimekua nikiamini kuwapa watu wengine kipaumbele, ni kitu sahihi cha kufanya na ndio uungwana na ubinadamu wenyewe. To some extent, bado naamini hivi.
Shida, ni kwamba, kwa miaka mingi—huko kuamini hivyo —ilinipelekea ku undermine kila kitu kinachonihusu mimi, na kuyapa mambo ya wengine kipaumbele kwanza. Hivyo utakuta, kabla hujafanya kitu, badala ya kujiuliza kama kitu husika kitakupa furaha…kama kuna namna kitakunufaisha, swali la kwanza lilokua linakuja kichwani, ni;
“Je, fulani atafurahi? Will they be proud of me?”

Na ikiwa thought-process yako iko hivyo, then kitakachotokea ni kujikuta unafanya mambo mengi ili mradi kunufaisha na kufuraisha watu wengine(wazazi, ndugu, jamaa, nk.), hata kama baadhi ya hayo mambo yanaweza yasikunufaishe. Hata kama yanaweza kukuumiza na muda mwingine kukuletea matatizo.
Hii yote ingekua haina shida sana kama hao watu wengine wangekua wanafikiria na kufanya hivyo hivyo kwako, shida ni kwamba binadamu tuko wabinafsi. Na wengi wetu, kwenye kila kitu tunachofanya tunajiwazia sisi kwanza kabla ya kufanya cinsideration ya actions zetu kwa watu wengine.
That said; qualities nzuri za kua nazo kama humility na empathy, zinaweza kukuharibia maisha entirely ukiziendekeza mno. I had to learn this the hard way. Again and again and again. Na hii inatuleta kwenye kisababishi cha tatu;
PEOPLE PLEASING

Technically; kama hujui kusema hapana, na kama wewe kwa kila kitu unaweka hisia, mipango, malengo, na mambo ya wengine kwanza kabla ya ya kwako. Tayari wewe ni people pleaser.
Kama nlivyosema, niko too self-aware, so mara nyingi ambapo nimekua nikifanya mambo ambayo yanawanufaisha wengine na kunikandamiza mimi, ndani kwa ndani nlikua nikijua sio kitu sahihi ya kufanya.
Kila ambapo mtu angekuja na issue ambayo nabidi niikatae, na najua nabidi niikatae, lakini sikuikataa, kichwani mwangu nlikua najua hii kitu sio sawa, lakini bado unajikuta unaendelea.
Nlipokua nabidi nifanye maamuzi, ambayo yangeninufaisha kwa kiasi kikubwa, lakini for some reason watu wangu wa karibu wakawa hawayapendi kwa sababu zao binafsi, nilikua najikuta naacha na kufanya wanavyosema, ili mradi tu nisiwakwaze. Japo ilikua inanikwaza mimi tena na tena.

Na ni kitu ilikua inaumiza kuona watu hawa ambao unafanya mambo yako kwa umakini wa hali ya juu, kuhakikisha hauwakwazi, walikua wanafanya vitu carelessly sana bila hata kujitafakari kwa sekunde kadhaa kua ‘hii kitu Frank ina muaffect vipi?’
So, kama nilikua nayajua haya yote, kama nlikua this self-aware; Kwanini bado ni kitu ambayo nimekua nikiendelea kufanya kwa muda mrefu tena na tena?
Kwanini imenichukua muda kuacha?
Kwanini nimekua nashindwa kujifunza kila nlipojikuta kwenye matatizo na majanga kwa sababu tu sikuweza kusema hapana, au kujiweka mbele kwenye mambo yangu?
Kwanini bado ilikuwepo hio hatia, na kujiskia vibaya kila iliponilazimu kufanya maamuzi magumu kidogo na kujiweka mbele?
Kwanini ziko nyingi hatari. Ikiwemo Kwanini sina majuto for all that’s happened. Na kwanini I’m unapolegetically myself now. Kwanini nimeamua kuandika kuhusu hili, haha. Ziko nyingi.
That said, tumalize kwa kwenda kwenye kiini cha andiko hili lote;
Katika Kitu Chochote Utakachofanya; Usiisahau ‘Kwanini’ Yako

Hapa nyuma kidogo nilianza kengeuka na kuanza kufanya vitu ambavyo sio vitu ninavyopenda kufanya, kwa kua nlianza kusahau the whole point ya ‘kwanini‘ nafanya mambo ninayofanya kwa sasa.
Kwanini siyafanyi kama nlivyokua nayafanya huko nyuma?
Kwanini nlianzisha hiki ki project cha Kainetics? Na hizi mambo za kuandika, na izo mambo mengine zote ambazo ninafanya…
Ila kwanza turudi kwenye ivyo visababishi huko juu;
KWANINI NILIKUA NIKIFANYA HAYO YOTE, HATA KAMA NILIKUA NIKIJUA YANANIUMIZA NA BAADHI NINAJIKOSEA?
Haha, Frank wa huko nyuma ingekua ndo umemdaka umuulize hayo maswali angekujibu accordingly kuendana na uelewa aliokua nao kwa wakati huo.
Ungemuuliza: Kwanini hujiweki mbele, na kila kitu unachofanya una consider hisia za watu wengine wote isipokua za kwako? Angekujibu: Kwa kua ni kitu sahihi cha kufanya, na kua sio mbinafsi.
Ungemuuliza: Kwanini unakua unashindwa kuweka mipaka kwenye baadhi ya vitu, na kusema hapana inapokubidi? Hadi unajikuta kwenye situations za kiwaki naa bado hujifunzi?
Haha hapa nadhani asingekujibu, angebaki anakodoa tu mi macho.
Ila ukiniuliza mimi kwa saa hivi, kwanini? Kwenye hilo swali la kwanza majibu hayatopishana sana. Kuconsider namna matendo na maamuzi yako yanaweza kuwa affect wengine (kabla ya kuyafanya) bado naamini ni kitu sahihi ya kufanya.

Japo kwa sasa, nitakwambia, kunamuda hizi considerations, unabidi uziweke kapuni na uwe na roho ngumu kidogo, kama hao hao watu unao waconsider, kama roles zingekua reversed wasingekufikiria hata kidogo.
Kuhusu hilo swali la pili, kwa sasa nadhani naweza kusema imekua hivyo ili nijifunze. Ninaamini ukikutana na jambo na ukashindwa kujifunza kitu lilichopaswa likufindishe, basi litakukuta tena na tena na tena, hadi kichwa yako ielewe.
Nadhani to some extent naelewa sasa. Na ndiyo sababu sijutii izo ma situations zote ambazo zimetokana na hayo maamuzi mabaya; huko kutojiweka mbele, kutosema hapana inapobidi, na izo utumbo za people pleasing. That’s why naweza kuzitafakari kwa saa hivi na kuishia kucheka mwenyewe.
Japo baadhi ya hizi mambo zimenipa ma depression ya kutosha. Nyingine zimenipeleka sehemu ambako sikujua naweza kufika. Nyingine zimenilaza njaa tena na tena, nyingine zikanichafulia jina, nk. Ila looking back in retrospect, sijutii. Kwa kua mwisho wa siku nimejifunza kitu.
Ifahamu Kwanini Yako

That’s all on my end. Ila nimeandika hayo yote ili niweze kuongelea point hii moja peke yake. Ifahamu ‘Kwanini Yako‘ na usiisahau, katika kitu chochote utakachofanya.
–Unataka ukasomee IT. Sawa, ila kwanini?
-Unataka uwe daktari, kwanini?
-Unataka ufungue biashara fulani? Kwanini hio biashara specifically?
-Unaenda kanisani ndio, ila kwanini unaenda?
-Sawa unaandika, unachora sijui, unaimba. Kwanini?
-Fulani kakuambia umuazimishe laki tano, atarudisha. Unaenda kumuazima. Ila kwanini?
–Unafahamu maovu ya fulani, lakini umeamua kuficha siri. Kwanini?
–Tabia ya fulani inakukera na anakuboa tu, lakini umekaaga kimya na unaendelea kumu entertain. Kwanini?
Hili ni moja ya swali muhimu la kujiuliza, kuliko maswali mengine yeyote utakapoenda kufanya kitu au kuchukua maamuzi.
Na ni muhimu kwa sababu nyingi, ila sababu kubwa ni litakusaidia kujua kama mambo unayoyafanya unayafanya kwa mihemko, na misukumo kutoka kwa wengine. Au unafanya, kwa kua sababu inatoka ndani kwa ndani. Nafsini mwako. Na hii inatuleta kwenye point ya pili;
Hakikisha Jibu La ‘Kwanini’ Yako Linatoka Ndani

Kama unaenda kusomea udaktari kwa kua nyumbani kwenu wamekulazimisha lakini sio kitu unachokipenda. Basi hata ufaulu, na upate mafanikio kwenye fani husika, hakutokua na fullfillment yeyote ile kama sio kitu ulijua unapenda kufanya.
Kama unaomba, unafunga, sjui una mantain picha ya utakatifu ili mradi watu wakuone, basi hauna tofauti na yule ambae kanisani hajaenda kabisa.
Kama umevaa ivo ulivyovaa, hata kama hupendi, lakini kwa kua tu unahisi fulani atakasirika ukivaa tofauti (simaanishi sasa ndo ukavae kiwaki haha) basi kwanini yako haina mashiko.

Kama umeamua kumsaidia fulani kwa kua unaogopa namna atakavyokuchukulia ukishindwa kumsaidia. Wakati unaelewa kule kumsaidia kwako kutakuharibia na yeye mwenye put in the same position hatoweza kujisadaka kama ulivyofanya, basi Kwanini yako haina mashiko.
Kama umeamua kuanza kuuza laptop na simu, kwa kua umeskia ndizo mambo Frank anafanya na zinampa faida. Na we hujui hata hizo faida zimetoka wapi na zinaenda wapi…haha hauna bahati.
Kama mtu kaja kakuambia naomba unifanyie hivi. Na unajua uwezo huo huna. Au haiko profitable, au kitu husika itakurudisha nyuma. Au kitu kimoja kikienda ndivyo sivyo then uko na msala heavy, Na kichwani mwako ukawa unayajua haya. Lakini bado ukaamua kufanya, ili mradi kumfuraisha/ku mantain urafiki sjui na mambo gani, haha huna bahati.
Point ni hakikisha, whatever you do, whatever you decide, basi sababu itoke ndani, kwenye nafsi yako.
That way, hata mambo zisipoenda zilivyobidi kwenda. Hata zikitokea zikakuumiza. Hata zikitokea zikaweje, hautokua na majuto. Kwa kua sababu yako ilitoka moyoni.
Hitimisho
Kwa miaka mingi huko nyuma, sababu ya kwanini nilikua nafanya hivyo nilivyokua nafanya haikua inatoka ndani. Na kwa sababu hiyo utakuta unajikuta kwenye situations mbaya zinazoumiza, na muda mwingine ni shimo refu ulilojichimbia mwenyewe, kana kwamba ni ngumu kutoka.
Na kwa kua sikujifunza mara ya kwanza, au ya pili au ya tatu, nimejikuta kwenye situations nyingi mbovu za kiwaki. Hadi somo liliponikaa kichwani.

Huko juu nimesema nlisahau kidogo kwanini yangu. Sababu ile kubwa inayonifanya nikeshe kwenye hizi hustle za hapa na pale, sababu nimepakia kichwa mavitu kibaooo mengine hata sijui kama nitakuja kupata manufaa nayo…
Kwanini nilifunga hii blog huko nyuma. Na kwanini nimeifungua upya…
Kwanini naandika…
Kwanini napenda izo mambo za ku interact na watu na kujibu maswali…hata kama haziko profitable…
Kwanini najitahidi niwezavyo kutokua mbinafsi, na kwanini nakaza inaponilazimu…
Kwanini tumeanza kwa kuongelea miaka, maamuzi, makosa yangu, hadi izo kwanini zenyewe…
Haha…kwanini hii post haina internal wala external links na izo mambo mengine kama izo?
Nlisahau. Ila to some extent nakumbuka now. Je, wewe unaifahamu ‘Kwanini’ yako?
Discover more from Kainetics
Subscribe to get the latest posts sent to your email.