Kuhusu Kainetics

Hi there, kwa mara nyingine—niite Frank Kai, na karibu Kainetics. Kama uko curious kufahamu Kainetics ni nini, naweza kusema ni blog niliyoanzisha maalumu kwa ajili ya kushare tips mbali mbali kuhusiana na mambo kadhaa yanayohusiana Mitandao, Digital Skills, pia Maisha, Biashara, Uchumi, Ujasiriamali na mengine mengi, kwa lugha nyepesi ya Kiswahili.
So ikiwa wewe ni kijana mwenzangu unataka jifunza mambo ya Web Design, au Programming, au IT kiujumla ila ufahamu pa kuanzia. Au kama ni mtu yuko fascinated na mambo za Graphics Design, Video Editing, Photography, Content Creation na mengine kama hayo basi Kainetics ndio sehemu sahihi.
Pia ikiwa labda unataka kujifunza kuhusu namna gani unaweza kutumia mtandao kujiajiri, kujiingizia kipato, au kutangaza na kuendeleza biashara ambayo uko nayo tayari, basi Kainetics ni blog ya kuweka karibu pia. Humu naongelea maswala ya Blogging, Affiliate Marketing, Freelancing, Vlogging, Dropshipping, Forex & Cryptocurrency Trading kwa kina na kwa lugha nyepesi inayoeleweka.
Mambo yote ninayoongelea humu, ni yale tu ambayo nimefanya au nina experience nayo, hivyo hata katika kuandika, najitahidi kuandika kwenye Point Of View binafsi.
Point kubwa na ya msingi ni kuweza kuelimishana, na kuelekezana mambo haya katika lugha hii hii ya Kiswahili ili hata kama ulikua unatamani kujifunza kitu fulani lakini hujui pa kuanzia, basi uwe na mwanga. Na kama ni kitu ambacho tayari una exposure nacho tayari, naamini yapo mawili matatu unayoweza kuyabeba pia. Hivyo, karibu.
Baadhi Ya Maswali Nayoulizwa Kuhusu Kainetics
Kainetics ni blog pekee ya Kiswahili iliyoanzishwa maalumu kwa ajili ya kufundishana, kuelimishana na kupeana mwanga kuhusu mambo mbali mbali ya kidigitali na yahusuyo mitandao ikiwemo; digital skills, digital marketing, kuingiza pesa mtandaoni na mambo kama blogging, affiliate marketing, nk.
Blog ya Kainetics imeanzishwa na Frank Kai, ambae ni kijana wa kitanzania whose main proffesion ni Web & Graphics Design, SEO na Digital Marketing na Blogging pia kama hobby.
Point kubwa ya kuanzisha blog hii ni kushare madini/ujuzi pamoja na experience kupitia posts na content ninazoshare. Ila ukitaka tufanye kazi pamoja, basi huduma ninazojikita nazo ni pamoja na Web Design (Kwa Wanaohitaji Tovuti Za Biashara, Pamoja na Blog,), SEO & Digital Marketing, Lastly Nafanya Branding pamoja na Graphics Design. Kuuliza maswali na general consultation ni bure, hivyo usisite kunicheck ukiwa na dukuduku.
Unaweza nicheck moja kwa Whatsapp kwa kugusa hapa, au kujaza form kwenye hio Page ya Mawasiliano. Instagram pia unaweza niDM @kaineticshq