Habari, kama wewe ni mtu ambaye umekua ukitamani kuweza kutumia simu/au laptop yako au hata ujuzi ulionao kujiingizia kipato online au hata kujiajiri kabisa lakini hufahamu ni vitu gani vya uhakika ujishughulishe navyo, basi moja ya hivyo vitu ni Freelancing—na katika makala hii nitaiongelea kwa kina.
Kwa kuanza na Freelancing ni nini, inafanyaje kazi, na ni namna gani unaweza kuanza kujiingizia kipato online kama Freelancer kwa mwaka 2025 kwenda mbele;
Freelancing Ni Nini ?

Kama ni mara yako ya kwanza kusikia neno hili, kwa lugha isiyo rasmi; Freelancing ni kufanya kazi kwa kujitegemea ukiwa nyumbani. Unalipwa na client mmoja au zaidi, kila mtu kwa wakati wake au wote kwa pamoja…na unalipwa kwa bei ulizojiwekea wewe (au mlizokubaliana) ili kuwafanyia kitu kwa kutumia ujuzi ulionao kuhusiana na kitu husika.
Yaani ukimfanyia kazi mtu au kampuni bila kukutana physically na akakulipa tayari hio ni Freelancing. Na mtu anaefanya Freelancing anaitwa Freelancer.
Ziko nyanja kibao ambako unaweza kujikita na kufanya Freelancing; na baadhi yake ni kama hizi hapa;
- Writing & Editing – Kulipwa kuandika, kukosoa makala, kufanya proofreading na mambo mengine mengi yanayohusisha kuandika.
- Graphics Design – Kama ni Mtaalamu wa Photoshop, Illustrator, Canva, InDesign, nk na unafahamu kudesign logos, mabango, business cards nk, unaweza jikita huku.
- Web Design & Programming – Kama unajifahamu uko vizuri kwenye maswala ya kuunda Websites, kucode, kuunda App za Simu, nk. Unaweza fanya Kazi hizi pia.
- Digital Marketing – Kama uko vizuri kwenye kuandaa content zinazoenda viral, kupangilia matangazo ya kwenye social media na mambo yeyote yanayohusiana na masoko basi unaweza base huku pia.
- Virtual Assistance – Kama ni mtaalamu wa kutatua changamoto za simu, au vifaa vya kielektroniki na unaweza saidia kampuni mbali mbali kutoa Assistance kwa wateja wao wanaokutana changamoto wakiwa wanatumia bidhaa zao basi unaweza fanya hivyo.
- Photography & Videography – Kama ni mtaalamu katika maswala ya photo editing, na kuedit video, composition, photo manipulation na mambo kaa hayo kazi hizo pia ni nyingi. Na nyingine nyingi…
My Freelancing Story
Moja ya vitu ambavyo nimevifanya kwa muda kabla sijaendelea kufanya mambo mengine ni hii Freelancing.
Na ndani ya miaka miwili ambayo nlifocus nayo, nimeweza fanya kazi na clients zaidi ya 80 kwenye platform tofauti, ila mainly ni hio UpWork na Fiverr. Overall nadhani nimeweza kuingiza karibia $7,000 kabla sijaacha kuifanya full-time nakuendelea na mambo mengine.
Kwa UpWork peke yake, account imeingiza $1,000 ikiwa imetokana na kazi 15+

Hio sio hela nyingi sana kiivo ila kwa Tanzania yetu na kama wewe ni kijana basi ni hela kubwa tu. Hivyo mambo mnegi nitakayo ongelea humu, nitaongea from experience na kuendana na uelewa wangu.
Unahitaji Kuwa na Sifa Gani Kabla Ya Kuanza Freelancing ?
Moja ya advantage za hii Freelancing, ni kwamba unaamua tu kua unataka ufanye kazi za aina fulani, na unaamua pia utakua unazifanya kwa kiasi fulani (rate) na unaanza zitafuta kazi husika na kufanya unapopewa. Ni simple hivyo na haina kona kona nyingi.
Ila changamoto ipo moja; Huwezi amia tu out of nowhere uanze kufanya Graphics Design kama hujawahi kabisa kufanya izo mambo na hata huzijui. Huwezi anza fanya kazi ambayo sifa zake huna maana ma freelancer wako wengi sana hivyo inakubidi kua sure kua kitu unachoenda kukifanya unakijua kweli, na sio kukijua tu; Unakiwezea.
Hivyo hio inatupeleka kwenye sifa yetu ya kwanza ya kua nayo, kabla hujaanza Freelancing;
1. Hakikisha Ujuzi Unao Wa Kutosha
Kama unaenda anza kufanya Freelancing, hakikisha unao ujuzi wakutosha kwneye kile kitu unachoenda kukifanya. Usidandie fani za watu.
Kama ni Graphics Design, hakikisha uko vizuri in theory na in practice pia. Unafahamu all the thought process inayo happen hadi logo inagengezwa, au business card, color theory, blocking, layout design, composition, typography na mambo mengine kibao kama hayo.
Hakikisha uko una uelewa wa kutosha na unazifahamu vizuri softwares zinazohusika kwenye kile kitu unachotaka uanze kufanya, na hakikisha uko vizuri pia kwenye kuzitumia.
Kama huna, tenga muda, jifunze. Kama unajua lakini hujui kwa kina, pia tenga muda kajifunze zaidi. Advantage ya kizazi chetu cha saa hivi ni karibia kila kitu kipo mtandaoni for free ukijua pa kukitafuta. Hivyo kama unawekaga bando kushinda TikTok na Instagram. Au wewe bando lako linaishia kwenye ku download movies na ma game,inabidi ubadili priorities.
Tenga hata mwezi au miezi miwili. Punguza kabisa kwenda huko TikTok na Instagram au kudownload izo movies and whatever inakulia bando…and instead. Ingia YouTube tafuta course za kitu unataka kujifunza. Na ujipinde uhakikishe unaiva au unakua na uelewa ambao ni above average.
Hivyo kama unataka kua Web Designer, tafuta course za Web Design. Kama unataka kua Graphics Designer, tafuta Course za Graphics Design. Ivo ivo kama unataka kujikita na mambo ya Editing. Tafuta relevant course, jifunze huku una practice mwenyewe hadi ifike hatua uwe na uelewa na karibua kila kitu in the given field.
Ili hata ukijitamkia kimya kimya kua ‘Nataka kuanza fanya Freelancing kama Graphics Designer’ basi yule wewe wa ndani yako hakucheki.
2. Hakikisha Una Basic Skills Nyingine Za Muhimu
Mara moja moja inaweza kukutokea ukawa unajijua kua unakifahamu kitu fulani kwa mapana na unajua kua uko vizuri kabisa kwenye hio sekta.
Let’s say ni mambo ya Production; uko vizuri sana kwenye kuunda beats, izo DAW (sijui Fl Studio, Ableton Live na Cubase zote unaziwezea vizuri tu) na upande wa Mixing, Vocal Processing sjui Mastering na makoro koro gani mengine yote uko vizuri kabisa…
Lakini akawepo mtu ambaye hayuko vizuri kama wewe…ukiskia mixing zake ziko average sana, mabeat yake mabovu mabovu ,mambo hazijapangiwa vizuri na bado akawa anaingiza hela na kupata wateja wa kufanya nae kazi kuliko wewe.
Hio inatokea mara nyingi kuliko tunavyodhani, na kwa muda mrefu ilikua inanitatiza. Ile kuona ‘Mbona niko vizuri kwenye hii kitu nayofanya lakini sipati kazi’
Na jibu ni simple. ‘Unahitaji zaidi ya huo Ujuzi’ wa Kawaida ili uweze kuuza na kujipatia Clients. Maana hio kujua tu, haitoshi.
Ujuzi wa kawaida hautoshi. Unahitaji ujuzi wa ziada
Hivyo basi, jifunze basic skills nyingine za mhimu, kama namna sahihi ya kuongea na watu. Maana unaweza kua vizuri kwenye kitu unachofanya lakini mtu asipende namna unavyo ongea.
Kuna mambo mengine ni ya kawaida sana, ila ni ya mhimu. Mambo kama namna unavyoandika meseji/jumbe zako. Je unaziandika vizuri with the right punctuation? Au ndo wale wanaandika sasa kama ‘xaxa‘
Jifunze namna ya kufanya negotiation, namna ya kutoa proposal zianzoeleweka, namna ya kujitangaza na namna sahihi ya kuuza huduma zako kwa your ideal customers.
Ukitenga muda na kujifunza hayo machache, ikiwemo hata namna ya kuwasiliana na watu tofauti tofauti tayari utakuwa umejipa advantage kubwa linapokuja swala la kuanza kuzitafuta na kuzifanya kazi zenyewe.
3. Lugha
Kwa Tanzania yetu, lugha iliyozoeleweka katika mazungumzo, iwe ya kibiashara au kawaida ni Kiswahili. Ila kwa bahati mbaya, on the global stage lugha hii haifahamiki kiivo.
Hivyo basi, uko na advantage kubwa kama unaweza kukizungumza kingereza. Kama una kielewa pia, na unaweza jielezea vizuri then uko na advantage kubwa zaidi.
Wakenya kwenye swala la Freelancing wametupita sana, na advantage kubwa walio nayo ni lugha. Hivyo hakikisha walau hii advantage unayo pia.
Na je kama lugha ni changamoto?
Ushauri naoweza kukupa ni jifunze. Ziko app nyingi za bure unazoweza tumia kujifunza lugha za kigeni, maarufu ikiwa Duolingo.
Pia unaweza tumia akili mtambuka/ artificial Intelligence kama ChatGPT kujfiunza Kingereza taratibu kwa usahihi.
Kitu kingine ni kama kingereza kinakuoiga chenga kabisa na unajijua hata kwa huko kujifunza bado learning curve yako itakua kubwa, basi unaweza tumia app zinazofanya tafasiri, kama Google Translate na kuziweka karibu, ikiwa unaongea na mteja/client ambae lugha yake huielewi vizuri.
NB: Haya mambo ya lugha, ni kama ukiwa Freelancer ambae unataka uweze pokea kazi hata kwa watu walio nje ya Tanzania (nitaongelea baadae)
Sema haimaanishi ni lazima. Unaweza kua tu Freelancer na ku base na clients wa Kitanzania. Inawezekana pia, ukijua namna ya kufanya iwezekane.
4. Uaminifu
Hii sipaswi hata kuiandika hapa ivi. Kama sifa hii inakutatiza, basi kujiajiri online ni ngumu. Maana ndio sifa ya kwanza kabisa unayobidi kua nayo kabla ya hizo nyingine zote.
Mitandaoni watu waongo waongo ni wengi mno, matapeli ni wengi pia. Na uswahili uko mwingi, kitu ambacho kinafanya kazi yeyote au hata biashara online kua tatizo au changamoto kubwa.
Watoa huduma wengi utakuta ni waongo waongo, na hata wateja wenyewe unawakuta ni waongo waongo haha hivyo ukiweza kua muaminifu, kufanya manbo yako kwa uwazi bila tamaa. Tayari utajizolea wateja wanaorudi (returning clients) na kupitia huo huo uaminifu wako utakua umejipa advantage ambayo wengi hawana.
Unawezaje Kuanza Freelancing? Hatua Kwa Hatua

Kufikia hapa nimeweza jitahidi kuongelea Freelancing ni nini, inafanyaje kazi, na ni sifa gani unabidi uwe nazo kabla ya kua freelancer (kutoa huduma zako mtandaoni)
Sasa nadhani ni muda tuanze kuongelea ni namna gani unaweza kuanza kufanya Freelancing, iwe wewe ni mwana chuo, au ni mtu ana kazi nyingine anafanya, au hata kama wewe ni mama wa nyumbani, hii ni kitu unaweza fanya. As long as umejitahidi kua na sifa nyingi kwenye hizo baadhi nlizotoa;
1. Chagua Ninche
Kwenye makala yangu nlikokua naongelea mambo ya kufungua blog nilielezea Ninche ni nini kwa upana. Ila kama ni mara yako ya kwanza kuliskia hili neno;
Kwa lugha isiyo rasmi, naweza sema Ninche ni kile kitu specific utakachokua unajihusisha nacho. Hio ndio Ninche.
Yaani ukiamua kua utajihusisha na mambo ya kuandika, basi iwe kuandika, au skills za ziada zihusiane na uko kuandika. Usichanganye.
Kama utaamua utakua unafanya mambo ya kutafsiri, au transcription, au labda ni mambo ya video, nk. Chagua kimoja.
Japo zipo baadhi ya vitu unazoweza fanya kwa pamoja maana zinaelekeana. Hivi ni zinaelekeana au vinaelekeana? Anyways…
Mfano; anaejishughulisha na mambo ya Video Editing, anaweza fanya Short Form Content, anaeza fanya pia Motion Graphics, na anaweza fanya pia mambo za 3D Animation, Rigging, Character Design, nk
Maana vyote vipo kwa aina moja ya Media: ambayo ni Video.
Hivyo, kabla ya kuanza, jiulize uko mbobezi kwenye mambo yapi, na kati ya hayo manbo yapi yanaelekeana? Na udeal na hivyo.
2. Amua Bei Zako
Kwenye Freelancing, wewe mfanyakazi ndio unaamua unafanya kazi kwa shingapi, na mteja anaangalia kama bei zako zinaendana na bajeti yake, na hivyo kufanya kazi na wewe au kutafuta mtu mwngine.
Unaweza angalia freelancer wengine wana charge shingapi, ili usijiekee bei za juu sana au za chini sana na kujiumiza.
Kama utakua unafanya kazi kwenye hizo platform za kimataifa, system ya malipo iko tofauti, maana utakuta wanalipana Per Hour. Hii inachanganya kidogo hivyo unaweza ifuatilia kwa kina, ila kwa kazi nilizotolea mifano huko mwanzoni hakikisha rate yako ni walau $7 hadi $35 per depending on the kind of thing utakua unafanya.
3. Hakikisha Uko Na Vifaa Vya Mhimu
Kama kazi utakazo kua unafanya zinahitaji laptop, then hakikisha una laptop. Japo kama ni beginner na unaanza, na muda mwingine laptop, au uwezo wa kua na hio laptop huna, basi unaweza anza na simu.
Kama laptop unayo, hakikisha software zote za mhimu uko nazo. Kama ni simu z hakikisha walau ina nafasi ya kutosha, na app za mhimu zote zinazoendana na kitu utakachokua unafanya, unazo.
4. Jisajili Kwenye Freelancing Sites
Hapa ni kuunda account kwenye freelancing sites husika. Ziko nyingi mno, na kila tovuti/kampuni ina taratibu zake ila zote mwisho wa siku zina approach moja.
Unaweza jisajili kama Client (mtu anaetafuta hao ma Freelancer) au unaweza jisajili kama Freelancer. Nadhani ndicho kitu tunachotaka.
Mambo ya kuhakikisha ni unatumia majina yako halisi, miaka ya kuzaliwa pamoja na picha iwe yako na inayoonekana vizuri.
Pia kwenye section ya Portfolio, unaweza andika kama kuna kitu umesomea kinaendana na skills zako, unaweza orodhesha hapo (mambo kama Major yako na chuo ulikosomea + mwaka)
Pia kama kuna kampuni au shirika umewafanyia kazi unaweza ongeza kwenye portfolio yako, kikunwa usiweke taarifa za uongo.
Ipo pia Bio ambako unaweza andika kwa ufupi, wewe ni nani, unafanya kazi za aina gani, nk. Kama unataka kuelekezana kwa kina kuhusu haya mambo ya kuandaa profile yako kama freelancer unaweza nicheck.
Baadhi ya Freelancing Sites nzuri unakoweza kujisajili;
- UpWork
- Fiverr
- Freelancer
- PeoplePerHour
- Toptal
5. Unda Portfolio/Website Ikibidi
Kama freelancer ambae yuko professional, unabidi ujiundie Social Media presence ambako mtu anaweza kupitia baadhi ya project zako ambazo umefanya tayari, kuoata mawasiliano yako, na mambo kama hayo.
Sio lazima sana kama unaanza, eti uanze na tovuti yako. Ila huko mbeleni ikikubidi, inapendeza kua na Porfolio.
Sema japo kua kutokua na website sio lazima sana kwa Beginner, hakikisha una links kwenye major social media platform zote kama Facebook, Instagram, Twitter na LinkedIn. Kama ni Designer, consider kua kwenye platform kama Behance na Pinterest pamoja na Tumblr.
6. Anza Na Kazi Ndogo Ndogo Kupata Reviews
Kwa kua unaanza, anza na tu kazi tudogo dogo hata kama hatulipi vizuri sana. Hutu tutakuzolea experience kwenye hizo platform husika kujua namna mambo yanavyokua nk.
Pia encourage wale wateja wako wa mwanzoni kuacha reviews kwenye profile yako maana hizo zitakusaidia huko mbeleni.
Hata kama mtu hakufahamu, akiona watu wengine wanakunenea mema, basi ni rahisi kufanya kazi na wewe hata kama hakujui na hamjafanya kazi kabla.
7. Changamana na Mafreelancer Wengine
Kwenye platform kama JamiiForums na Twitter wako watanzania wanaofanya hii freelancing, na baadhi wanaongelea , kushare experience, changamoto na mambo kama hayo. Unaweza kuwa follow ili uweze kujifunza kwa kina kuhusu mambo mengine mengine ambayo hata hayaongelewi kwa urahisi kwenye community za Kiswahili.
Baadhi wana Channels na ma group ya Whatsapp, changamana huko ili uweze pata ma ujuzi na ikibidi hata watu unaoweza wauliza maswali ukikwama.
Kwa JamiiForums huko mara moja moja hutokea threads zinazoongelea swala hili, ivo ni vizuri kupitia mara moja moja na kubeba mi ujuzi ikitokea mtu ametoa nondo.
8. Kua na Growth Mindset
Huko mwanzoni nimesema kua kabla ya kuanza jitahidi kuhakikisha uko na skills za kutosha kwenye hio ninche yako. Ila bado haimaanishi ndo utakua bora sana kuliko wengine. Na isitoshe ukiwa ni beginner na hujafanya kazi na mtu, na account ni changa, itakuwepo changamoto kidogo kuanza kupata pata kazi ila haimaanishi ndio hupati.
Ivyo jiwekee malengo, goals & milestones na fanya kazi kuzifikia hizo milestone umejiwekea.
Hata kama uko pro, usiache kuendelea kujifunza na ku adapt kadri unavyokua.
Kama utaanza na simu, hakikisha moja ya goals zako ni kua ukipata hela kidogo mwanzoni unahakikisha unanunua laptop.
Kama umeanza na laptop, moja ya goals zako ni kuhakikisha unapata laptop ambayo ni bora zaidi ya hiyo unayotumia.
Point ni usisahau kuwekeza kwako, wekeza kwenye vitendea kazi, na kwenye kujifunza, and the investment will be worth it.
Mara moja moja pia utakutana na clients wagumu, wengine wakorofi, wengine wasumbufu na mambo kama hayo. Inaweza kukuwia ngumu kupata hata izo kazi, ila inabidi isikukatishe tamaa. Maana changamoto ndogondogo kama izo ndizo zinakujenga and overtime unazoea.
Baadhi Ya Changamoto Zinazowakumba Mafreelancer wa Kitanzania

Freelancing ni kitu inafanywa na watanzania japo sio kwa wingi kiivo kwa kua mambo ya mtandaoni bado hayana exposure sana. Moja ya sababu kwanini kama ni mtu unaejikubali kua una skills fulani, basi inafaa uipe consideration.
That said, bado zipo Changamoto kibao zinazowakumba ma freelancer wa kitanzania, ila almost zote zinatatulika, lah sivyo nisingeandika makala ndefu namna hii.
Baadhi ya hizi ma changamoto ni;
Internet
Sehemu nyingi bado internet inasumbua, na clients wengi utakaokutana nao watakua wakuwasiliana mtandaoni.
Ivo hakikisha swala la mtandao halikusumbui na umeweka kila kitu sawa kwenye idara io kabla ya kuendelea.
Huko mbeleni ikikubidi, chukua Portable Wi-Fi ili kuraisisha workflow yako nzima.
Namna ya Kupokea Malipo
Changamoto nyingine ni njia rahisi na pendwa ya Paypal kwa Tanzania haifanyi kazi.
Tanzania tunaruhusiwa kutima tu hela ila kupokea bado ni kipengele. Sema bado zipo namna unavyoweza izunguka hii changamoto.
Unaweza fungua account ya Payoneer, Skrill au ikbidi kupokea malipo moja kwa moja kwenda bank.
Muda
Changamoto nyingine ni kama sio mtu aliezoea kukesha basi baadhi ya kazi zinaweza kukutesa kidogo. Japo nayo hii ina depend na clients wako wanatoka nchi gani.
Kama ni watanzania au wako East Africa hii basi hakuna shida sana. Ila kama ni wa nje, muda mwingi tunapokua tumelala wao ndio wanakua macho ivo itakubidi kua macho kwa muda wao.
That said, kama ni mwanachuo, mwanafunzi, au una kazi inayokubidi kuwa macho mchana, hakikisha unapangilia ratiba yako ili mambo yasiharibike.
Itimisho
Nadhani kufikia hapo hii kitu nimeiongelea kwa kina kadri niwezavyo. Hivyo kama ulikua umeshawahi sikia freelancing ni nini ila haijawahi kuelezewa vizuri kwa lugha unayoelewa, au hata kama ulikua hufahamu Freelancing ni nini; basi hii ndio freelancing kwa mapana yake.
Feel free kunicheck ukiwa na maswali, dukuduku au maoni. Na pia unaweza comment kabisa hapo chini. Asante.
Discover more from Kainetics
Subscribe to get the latest posts sent to your email.