Hi there, karibu kwenye makala hii ambapo nitaongelea kwa kina(kidogo) aina kuu tatu za watu ambao unabidi uwakate kabisa na kutoruhusu wawe karibu na wewe na pia nitaelezea ni namna gani unaweza kuchagua kwa usahihi watu wa kuwaweka karibu yako.
Binadamu by nature ni social beings. Kwa kusema hivi, namaanisha ni moja ya viumbe ambao tuko programmed ku-survive kwa kuchangama/kujumuika na wengine.
Baadhi ya hii mijumuiko ni ile ambayo tunaikuta tayari toka tunapozaliwa na hatuna usemi kiivo kwenye namna ilivyo na namna tunavyohusiana nayo;
Mfano; mtu huwezi chagua familia unako zaliwa. Huwezi chagua Wilaya, Mkoa, Kabila au Nchi unakozaliwa. Ni inatokea umezaliwa na unakua sehemu ya Jumuiya husika by default.
Upande wa pili, zipo connections ambazo ili zitokee tuna usemi kwa asilimia kadhaa, na nyingine kwa asilimia zote. Una usemi kwenye kuchagua Hobby unazozipenda, Role Models, Chakula, Vitu Vinavyokuvutia, Mwenza wako wa Maisha, Marafiki, nk.
Utangulizi

Kila kitu tunachokichagua, automatically kinatuweka kwenye Jumuiya moja na watu wengine ambao wamekichagua kitu husika. Ukiamua kua wewe ni Shabiki wa Simba, automatically uko Jamii moja na mashabiki wengine wa team ya Simba.
Ukiamua kua unapenda kuchora, basi wewe na wachoraji wengine mko jamii moja, nk.
Kwenye baadhi ya scenarios, hatuchagui vitu, bali watu wenyewe na hizi ndizo scenario nitakazo ongelea kwenye andiko hili. Siendi kukwambia uchague aina gani ya marafiki, au watu ambao unawaweka karibu; maana zipo sababu nyingi mno zinazo mfanya mtu na mtu wawe karibu, na sababu hizi zinatofautiana kwa kila mmoja wetu.
Ila, kwenye makala hii nitaongelea watu ambao, no matter what, and for the sake of your inner peace, hupaswi wachagua au kuwaruhusu wakuzoee. Kama baadhi ya haya maneno yatakua mageni, nitaongelea pia maana yake, sifa zao, na kwanini hupaswi kabisa kuruhusu wakuzoee.
Watu hawa ni Narcissists, Toxic People & Emotional Manipulators. Bila kupoteza muda, tuanze;
Yaliyomo
1.Narcissists

Nimetumia muda mrefu kidogo kujaribu kufikiria neno hili kwa Kiswahili linakuaje, nikashindwa kupata neno sahihi. So nimebidi niliandike kama lilivo(kama unafahamu kiswahili chake feel free kunijuza kwenye comments)
Kama ni mara yako ya kwanza kusikia neno hili, naweza kusema kwa ufupi Narcissist ni mtu ambae anajiona yuko bora zaidi ya wengine, na sio kujiona bora tu, yaani kujiona bora kwa kupindukia. Ni mtu ambae anapenda sana sifa/kutukuzwa na hawezi kueka kitu chochote mbele isipokua yeye mwenyewe, kwa lugha nyingine naweza sema—mbinafsi.
Baadhi Ya Sifa za Narcissists
- Kujikuza — Kwa kujikuza, namaanisha kujipa umuhimu uliopitiliza kwenye maisha ya wengine. Ni wale watu ambao wanaamini bila wao wewe sio kitu.
- Wanakosa Empathy/Kutokujali — Narcissists ni ngumu kujali mambo ya wengine isipokua ya kwake. Furaha, Huzuni, na Changamoto za watu wengine kwake anachukulia poa na kama vile si kitu ila anataka hizo hizo hisia zikiwa kwake zipewe kipaumbele.
- Kupenda Sifa — Narcissists ni watu wapenda sifa. Kama anajuana na mtu anaehisi ni wa maana au kama kuna ka kitu anajua au kuna kitu kamfanyia mtu atatumia nguvu kubwa kuhakikisha dunia nzima inajua.
- Kuwatumia Watu Wengine Kutimiza Mambo Yao — Hawa watu wanajiweka mbele kwanza na hukosa utu. Kama kitu fulani kinaweza kukuchafua na kusamfisha yeye yuko heri akifanye, wewe utajijua. Kama kuna kitu unaweza kumfanyia, ndio the only time atakuweka karibu ila ukishamfanyia kile anataka au ukishindwa kukifanya basi anabadilika.
- Entitlement/Kujikuta Miungu Watu — Wanaamini wanabidi wapewe ka special treatment popote wanako enda. Hii sitoiongelea kwa kina.
- Gaslighting — Moja ya utumbo walio nao hawa watu ni kutakaa kukaa wanabadili ukweli kukuaminisha uko kwenye makosa kila wanapokosea wao. Ni ngumu sana kukiri makosa yao na unapowadaka wakashindwa jiteteta basi huenda kutafuta huruma ya watu wengie.
- Hawapendi Kukoselewa — Hawapendi kukosolewa au kuambiwa ukweli. Ukiwachana makavu, badala wajitafakari na kujirekebisha wanakimbilia kuhisi unatafuta ugomvi, au unawavuniia heshima au kuwatukana.
- Mahusiano Ya Uongo/Kinafiki — Utakuta wanajuana na watu kibao na muda mwingine wanafanyia acts za wema watu tofauti. Ila ilimradi tu ionekane wanajuana na watu na ivo vitu wanavyofanya viwe tu kupata kitu cha kuongea/kujioshea kwa wengine.
Kama unafahamu mtu yeyote mwenye sifa za hivi na ni mtu wako wa karibu muweke mbali kabisa na usiruhusu asikuzoee.
2. Toxic People

Toxic people ni wale watu ambao wapo tu kuleta negative energy kwenye kila kitu, na kuwaharibu wengine kisaikolojia. Kam uko na mtu ambae unamfahamu ambae unajua tu akiwepo hata kama ulikua una furaha basi furaha inapotea ghafla. Yaani kila kitu kwao wanawaza mambo negative tu, kukutia tia mi hofu,ushinde na mi stress muda wote.
Baadhi Ya Sifa Za Watu Toxic
- Wako Negative Muda Wote — Ni ngumu sana kufanikia mafanikio ya wengine. Chochote utakachofanya watatafuta kitu cha kukusoa.
- Manipulative – Nao kama ma narcissists ni watu ambao wanapenda kutumia watu wengine kukamilisha mambo yao, kubadili badili ukweli na mambo kama hayo.
- Ngumu Kukiri Makosa Yao — Wao wanaamini hawakosei, wakishindwa kupata namna ya kujitetea watatafuta mtu wa kumlaumu ili mradi tu wasikiri makosa yao wenyewe.
- Wivu & Ushindani — Hawa ni watu ambao wanapenda ushindani na kujilinganisha na wengine. Sio ajabu Mafanikio ya watu wengine yakawalza macho. Ni ngumu kufurahia mambo mazuri yakitokea kwa wengine, wako na roho ya kutu japo ngumu sana kukiri.
- ‘Umama’ — Hii kitu naiita umama, ila kwa kingereza tunaweza sema passive-aggressiveness. Ni watu ambao ni ngumu kua open wakikwazika, lakini watatumia njia za ovyo ovyo kukufikishia ujumbe. Matani ya ajabu ajabu, kujaribu kukudharirisha, sarcasm , au kukunyamazia kila kila panapotokea tatizo. Instead of addressing the issue.
- Kunyonya Furaha Ya Wengine — Yaani uwepo wao sehemu unaondoa furaha. Kubonga nao kidogo tu, yaani kufikia muda wanaepa unakua unajihisi ovyo ovyo, huna furaha au umechoka zako.
- Kupenda Kutafuta Huruma Kwa Watu — Kila pakitokea kitu, instead of fxing the issue, au kujirekebisha wanakimbilia kwa watu wengine kuanza kujielezea na kuonesha wao ndo wamekosewa, muda mwingine bila hata kuulizwa.
- Umbea — Hawa ni watu ambao kila ukikutana nao wako na story kuhusu fulani, ziwe nzuri au mbaya. Yaani ni watu ambae wanapenda kuongelea mambo ya watu wengine. Na muda mwngine kukuchikba kutaka kujua ya kwako, hata yasio wahusu.
- Kutoheshimu Mipaka Ya Wengine — Kwa sababu ipo hio kitu ya kujiona sahihi kila muda. Huamini mambo yao ndio yako sahihi ivo hawaheshimu mipaka na mambo ya wengine. Iwe ni imani, mawazo au hata kujichomeka kwenye mahusiano yako na watu wengine yasio wahusu wao.
Kama unafahamu watu wa hivi, na uko nao karibu waondoe na usiruhusu wakuzoee kabisa.
3. Emotionally Manipulative People

Hawa ni watu fulani wa ovyo na muda mwngi huwa na sifa za hao ma narcissists na hao toxic people. Ni watu fulani ambae hutumia tu tricks na tu michezo twa kisaikolojia kuwaingia watu wengine ili wapate wanachotaka, wawafanye wafanye wanachotaka au tu wawe wana wacontrol.
Nasema ni wa hovyo maana hutumia vi njia vya ovyo na kufanya victims wao wabaki wanajihisi hatia, au wana makosa kila wakikengeuka na mipango yao ya ovyo.
Baadhi Ya Michezo Ambayo Hutumiwa Na Hawa Watu
- Gaslighting — Hii ndo ile unakuta wanakufanya uhisi kama vile huna kumbukumbu au matukio unavyoyakumbuka sivyo yalivyotokea. Mfano; “Me sikusema ivo, utakua na wenge.” au “Hayo nayo yametoka wapi, mbona sikuiongea kama ulivyoichukulia…”
- Kukujengea Hatia — Kila unaposimamia misiamo yako, kukataa mambo yao ya kiwaki, nk. Utakuta wanatumia kauli kama “sikutegemea ungesema/ungefanya ivyo baada ya mambo yote nliyokufanyia”
- Kutia Huruma — Kila unapowaweka kikaangoni wakakosa comeback ya maana watajaribu kutia huruma, ili ujisikie vibaya au uachane na topic husika. Mfano; “Yaaani ungejua mambo ambayo ninapitia alafu na wewe nakuona unaleta hayo mambo yako. Ungejua ungeyaacha tu…”
- Kukukaushia Usipoendana Na Mambo Aliyokua Anataka — Unakuta anaacha kukusemesha au kujibu meseji, nk. Ilimradi uanze kujiuliza umekosea wapi, nk.
- Kupindisha Ukweli — Hawa nawaita watu wa ovyo kwa kua ni watu wanaopenda kupindisha pindisha ukweli ili mradi wajijengee picha ya kua sahihi kwa watu na hata kwako. And sometimes unakuta kwa kua wamezoea kuishi kwa kubadili badili ukweli wa matukio hadi wao wanaamini uongo wao wenyewe.
Kama unafahamu mtu yeyote mwenye tabia za namna hii; ni mtu wa kumkata kabisa kutoka kwenye maisha yako kama unajiheshimu na unaheshimu amani ya nafsi, roho yako na afya yako ya akili.
Tafakuri

Aina izo tatu za watu ambao nimewaongelea kwenye makala hii, tunaweza kuwaweka kwenye kundi moja; kundi la watu ‘Negative‘. Na hawa watu negative, kwa desturi zetu za ki Tanzania, ni wale watu ambao wana mambo hasi-hasi. Iwe ni fikra, matendo, au mawazo.
Watu wadanganyifu, wachonganishi, wadanganyaji, wambea, wazee wa masimango, watu wasiokiri makosa yao— hawa wote wanaangukia kwenye kundi moja; la Watu negative.
Na dhumuni la andiko hili sio uhakikishe unajitenga na aina tatu ya hao watu negative alafu hao wengine uendelee kuwaweka karibu, hamna. Kwa namna nyingine niseme unabidi kuhakisha kua huwi na aina yeyote ya watu wenye mawazo, matendo au fikra hasi, ila hizo aina tatu zilizo kithiri ndizo nitakazo zungumzia.
Kwanini Ni Muhimu Kujiweka Mbali Na Aina Hii Ya Watu? (Watu Negative)
Sababu kubwa ni ili uweze kua na amani ya moyo. Na hata kuhakikisha afya yako ya akili haidumai kisa tu aina ya marafiki, ndugu au jamaa ambao umeruhusu waendelee kujichomeka kwenye maisha yako ikiwa their energy iko so low na inakudidimiza.
Hio ‘Kwanini’ ni ngumu kuitoa saa hivi, ila impact ni kubwa. Siku ukiamua kujiengua na aina hio ya watu ambayo tumewataja kwa huko juu (hao wanafiki, wachonganishi, wasenganyaji, nk) tofauti utaanza kuiona almost immediately.
Kuna nuru ndani yetu inapotea kadri tunavyozidi kuruhusu aina fulani ya watu wawe karibu yetu.
Kama una watu ambao wanakufanya kila muda uchague maneno ya kuongea, watu ambao kila kitu kwako wanaona ni makosa hata pale unapofanya kitu kizuri hawaoni; watu ambao wako na uwezo wa kukukosea tena na tena na kutegemea samahani itoke kwako, watu ambao wanakusema mambo ya ovyo kwa watu lakini wakiwa na wewe wanakuchekea…na hao wengine wenye tabia kama izo; huwezi kua sawa kifikra, na mtu yule ambae hajazungukwa/kajiengua nao.
Swali likiwa ‘Kwanini ni muhimu kujiweka mbali na aina hii ya watu?‘ sababu ziko nyingi sana, na nyingi ili uzielewe ni mpaka ujiengue.
Ila swali likiwa ‘Kwanini uendelee kuwaweka watu negative na wenye tabia za ovyo karibu?‘ Sababu za maana hazipo. Hivyo;
Kwanini Wengi Wetu Tunaendelea Kuwaweka Karibu—Japokuwa Uwepo Wao Unatukwaza?
Hapa for some reason sababu zinakua nyingi ghafla. Mtu unaweza kumuuliza, ‘Kwanini unaendeleza urafiki na fulani ikiwa unajua anakuchafuaga kwa watu?‘ akakujibu tu kwamba it’s complicated.
Anaweza kuwepo mwanamke mtaani mnafahamu huwa anapigwa na mmewe, na mnaweza kumuuliza kwanini unabaki hapa hivi ikiwa mumeo anakuumiza? Majibu atakayokupa ni yale yale. Yasipo kua yale utaambiwa huwezi kuelewa.
Huyo mtu ambaye hayukogo accountable na matendo yake, ambaye huwa anajiona sahihi no matter what?
Huyo mtu ambae anatumia kila nafasi anayopata kukukandamiza na kukuona hufai…
Huyo mtu ambae mafanikio yako, au wewe kupiga hatua ina mkwaza…
Huyo mtu ambae, ukiiisimamia misingi yako, au kumchana makavu akikosea, na yeye badala ya kusikiliza unachojaribu kumwambia anaanza kukuona uma dharau, au majivuno…
Ukiulizwa kwanini bado unaruhusu aendelee kukuzoea, kufahamu mambo yako yanavyoenda, kuwa karibu yako wakati unajua matendo yake sio, na yanakukwaza; Jibu lako litakua lipi?
Binadamu ni Social Creatures (Majibu)

Mwanzoni kabisa mwa hii makala nimesema kwamba kujumuika na wengine iko programmed deep in our existence kama sehemu ya survival. Na muda mwingi watu hawa negative hutumia muda mwingi na nguvu kubwa kujiweka karibu yetu kana kwamba kujing’oa huwa ina feel kama unakosea.
Uvumilivu
Na kwa kua sisi ni social Creatures, muda mwingi huwa tunajidanganya kua tunaweza kuwavumilia na mabaya yao kwa kua tunashawazoea hivyo hawatushtui na ‘tunajua namna ya kuishi nao.’
Hii kwa asilimia zake inaweza kua sawa, ila ina maanisha badala ya kuchagua amani ya moyo na kujijengea environment sahihi, na kujiweka mstari kwanza, tunajitoa sadaka ili tusikwaze mahusiano ya muda mrefu na hawa watu wenye mambo ya ovyo.
Social Programming
Hii social Programming, pia inaweza kukufanya uone tu kwamba mmetoka mbali, na kujitahidi uwezavyo kuyaona yale mazuri tu, huku wenzio kwako wanajaribu wawezavyo kuyaona mabaya yako tu. Na wakiyakosa, kutafuta, kutengeneza au kubuni ya kwao.
Kung’ata na Kupuliza
Kitu kingine, watu wengi wenye tabia hizi za ovyo, wana ile kitu ninayoweza kuita ‘kung’ata na kupuliza’ . Mtu mchonganishi, mnafiki na mbea ni watu ambao hawajui kuchagua upande. Watataka wawe in good terms na wewe, na at the same time wajaribu kua upande wa pili pia.
Akikusema vibaya huyo ndipo ataongeza ukaribu maana nafsi yake muda mwingi inakua nahofu na atatamani kujua kama unafaham mambo aliyoongea huko au hujui. Akigundua hujui ataendelea na tabia yake.
Mtu anaekunafikia, na kukusimanga nae ivo ivo. Wote huwa hawana confidence ya kuongea mbele yako kile wanachokiwaza kichwani mwao. Hivyo mabaya yote na mambo ya ovyo watakayokua wakiongea na kufanya watahakikisha wanafanya ukiwa hujui, nabhuwa wanaenda chafua sehemu ambako sanajua ni ngumu taarifa kukufikia kwa urahisi.
Tabia hii ya kufanya ubaya, huku wakiendelea kukufanyia wema inaweza kua overwhelming kufanya maamuzi magumu. Maana kitu unachokua na first hand experience nacho ni ule wema au ule ukaribu unao oneshwa (kupuliza) ila yale mabaya hutokea suddenly na kwa umbali maana ni mambo ambayo wanafanya nyuma ya pazia na kufahamu kwako kwa asilimia kubwa huwa ni kwa bahati mbaya (kung’ata) hivyo hii inaweza endelea mfanya mtu aendelee waweka karibu kuendana na how good they are at acting.
Maigizo
Na hio hio acting/maigizo ndio sababu nyingine kubwa ambayo inafanya wengi wetu tuendelee kua na hawa negative people karibu yetu ilihali tukijua sio watu sahihi. Narcissists, Toxic People na Emotional Manipulators ni watu ambao kwa asilimia kubwa wanaishi maisha fulani ya kuigiza, na hutumia nguvu kubwa kuiaminisha jamii kua wako tofauti kabisa na vile walivyo.
Mtu ambae hakili makosa yake, na ni mchonganishi atajitahidi awezavyo kufanya vitu ambavyo vitakufanye uonekane uko kwenye hatia tena na tena kwa watu, hivyo unajikuta mara nyingi unakuta the victim anashindwa jieungua/jitetea au kuweka ukweli ulivyo.
Na in some cases, the manipulation inakua kubwa kana kwamba unaweza anza kuamini uongo wao na kujihisi uko kwenye makosa hata kama uko sahihi;
Sentensi kama…
“Yaani umekaa ukajitafakari, ukaona unachoongea uko kwenye usahihi?”
“Kwa mambo ambayo nimekufanyia nilikua sitegemi ungesema kitu haka hiki“
“Haya, uko sahihi“
“Kama unajiona uko sahihi, ni sawa”
…na nyingine nyingi hutumika na aina hii ya watu wa ovyo kukujengea hatia, na kukufanya ujiskie vibaya, au uanze ku question kile ulicho ongea, hata kama ulikua kwenye usahihi.
Na kwa kua mtu anajengewa hizi hatia tena na tena, ni rahisi kufanywa aonekane mbaya kwa watu, au ajihisi anakosea kila atakapo amua kujiengua.
Strong Ties
Lastly sababu nyingine ambayo ni kubwa na recurring kwenye maisha yetu ya kila siku, ni sana sana most of toxic situations tunazokua nazo, hutokea kwa watu ambao wametuzidi umri, watu tunaowaheshimu, na muda mwingine ndugu, hivyo tunaam kuvumilia all the wrong doings kwa sababu ya heshima maana kila utakapotaka jielezea, jiteteta, jisimamia, na maneno yako kuanza kuleta maaana, resolution wanayokuja nayo inakua kua hauna heshima, una dharau, nk.
Sema, mwishowe wa siku inabidi uamue kujichagua wewe kwanza, kujiengua na kutafuta mahusiano ambayo yako positive. Na unabidi ufanye hivo hata kama itakua ngumu, au utajiskia vibaya, nk.
The fact that ita feel hivo ni moja ya sababu kwanini unabidi ujiengue. Maana mahusiano sahihi, na watu sahihi hawapaswi kufanya mambo yafeel complicated kila tunapobidi kufanya maamuzi yanayolenga furaha yetu binafsi + amani ya moyo.
Namna Ya Kuchagua Watu Sahihi na Kujenga Mahusiano Chanya

Ingekua ni summarizd hii section kwa sentence moja tu, ningesema tu Quality over Quantity.
Quality Over Quantity
Moja ya mambo ambayo unabidi kuyaweka sawa ni kuhakikisha uko na watu wachache wa maana na wa faida.
Kama binadamu, huwezi kupendwa na kila mtu. The toxic, the narcissists, and the emotionally manipulativd people ndio hutumia nguvu kusafisha imagebyao waonekane wema na watu wa maana sana kwa watu. Na ukiwa ni mtu ambae hutaki shida na kila mtu, yeyote ajaye basi unamuweka karibu tayari uko more probable kujikuta ushachangama na watu wa ovyo.
Hivyo lengo lako kubwa na la muhimu, lisiwe kua na marafiki kibao, upendwe na kila mtu, au kua mtu fulani ambae mtu yeyote anaweza kumzoea akitaka. Hamna.
Inabidi kua mtu ambae ana watu wake wachache, wa faida na wa maana. Ambae anajua akiwahitaji watakuwepo kwa niaba yake no matter what, nae atafanya ivo ivo kwao pia.
Haimaanishi uanze kufanya mambo ya ovyo pia kwa kisingizio hicho cha huwezi kupendwa na kila mtu. Na haimaanishi uache kuongea na watu, au uanze kua na roho mbaya au mtu wa ovyo pia. Hamna, endelea kua hivo hivo, ila kua na mipaka kwenye watu unao ruhusu wawe karibu yako/wakuzoee.
Chagua Watu Ambao Wanakupa Amani Ya Moyo
Chagua watu ambao wanakupa amani ya moyo. Watu ambao hawahitaji ujielezee sana kukuelewa. Watu ambao wako na wewe kwenye wakati mbaya wako, na kwenye wakati ambao mambo yanakunyookea.
Chagua watu ambao wanakufanya uwe wewe. Watu ambao hawakufanyi ukae kinyonge muda wote.
Chagua watu ambao hawakufanyi uwe mguu pande(attention) muda wote. Watu ambao hawakufanyi uchague maneno ya kuongea. Uchague mambo ya kuwaficha na ya kuwaambia. Chagua watu ambao wanakufanya uwe wewe. Watu ambao hawakufanyi ukae kinyonge muda wote.
Chagua Watu Ambao Wanataka Ufanikiwe
Kama umezungukwa na watu ambao wamezoea kukuona kwenye shida shida tu na mambo yako yakianza kukunyookea kidogo wanaanza kukwazika (hata kama ukiwa kwenye hizo shida zako wanakusaidia)
Kama umezungukwa na watu ambao wanafurahia the weak you, the poor you, the unsuccessful you. Basi hio ni ishara moja wapo ya kujiondoa kwenye hio circle na kutafuta watu ambao wanatak kukuona ukipiga hatua. Ukifanikiwa.
Chagua Watu Ambao Hawapendi Ushindani
Ushindani ni chanzo cha chuki, umbea, na huo unafiki maana vitu hivi hutokana na kitu inaitwa wivu. Ukiwa umezungukwa na watu ambao kila kitu kwao ni mashindano basi jiondoe mapema sana.
Kama rafiki yako anaweza kukununia ukipata marks kama zake shuleni, au akakununia kisa umeanza kufanya biashara kama anayofanya yeye.
Au kila kitu unachofanya nao wanataka wafanye kwa kushindana nawez basi jiengue hapo. Tafuta watu ambao mafanikio , hustle zako na whatever you do hawaitafsiri kama vile unataka kushindana.
Chagua Marafiki Ambao Wako Tayari Kukuchana Makavu Ukizingua
Ni kitu kidogo, lakini ni kitu cha muhimu sana. Mtu mnafiki/anaekusimanga/mmbea ni yule ambae anapeleka mabaya yako kwa watu. Lakini rafiki wa kweli ni yule ambae hayo mabaya yako atayakuambia akiwa anakuangakia usoni, na kukwambia ujirekebishe, na huko kwa watu atalitetea jina lako. Iwe upo , unaona au unasikia au iwe haupo hata.
Rafiki wa kweli ni yule ambae ata expect the same kutoka kwako pia. Ukiwa na rafiki ambae akikosea ukamchana makavu anaanza kuichukulia kama vile umemtukana, au umemvunjia heshima. Au yeye ukikosea hakwambii anaendelea kukuchekea ila kwa watu anaenda kukusema na kukucheka basi huyo sio rafiki. Uko na kikaragosi, na jiondoe hapo na usiangalie nyumanwala kujutia maamuzi yako.
Hitimisho

Kuchagua watu sahihi, na kuwakataa/ kuwaweka mbali wale wenye mambo ya ovyo, hasi(negative) ni moja ya mambo ya muhimu, ya msingi na maamuzi magumu unayobidi kuchukua kama unajiheshimu, na una jali afya yako ya akili pamoja na furaha yako.
Hakikisha watu ambao wako karibu yako, ni wale watu ambao wanakufanya usijutie au kujiskia vibaya kua wewe hivo ulivyo. Wawe watu ambao wanafurahia kukuona ukifanikiwa, watu ambao hawataogopa kukwambia wakiona una kengeuka. Watu ambao hawaogopi kukwambia maneno magumu kusikia. Watu ambao mnaweza ongea mambo ya maana na kupandishana madaraja kutoka hatua moja kwenda nyingine.
Sio watu ambao wako na wewe wakihitaji kitu tu, sio watu ambao wanakasirika ukiwakosoa na kuwachana makavu. Sio watu ambao wanafurahia kukuona mnyonge na mambo yako yakiwa hayaendi. Sio watu ambao watakucheka na kukusema huko kwa watu pale unapokosea badala ya kukufuata kukuambia. Sio watu ambao watakusaidia, na kisha kwenda kujitangaza huko waonekane wa maana. Sio watu ambao kila kitu watakachokufanyia ni kwa kua kuna kitu wanategemea in return. Sio watu ambao watasaidia kukuchafua na bado kuendelea kukuchekea wakikuona.
Usichague watu wenye sura mbili. Chagua watu wachache wa maana na wa faida. Maisha ni mafupi kukubali kuendelea kuzungukwa na watu wanao kudrain energy, na kukufanya uishi kwa mahesabh mazito as if unacheza Chess. Asante.
Discover more from Kainetics
Subscribe to get the latest posts sent to your email.
Umeongea mambo sahihi sana
😊🤞