Blogging na kuandika kiujumla— kama ni kitu ambacho unakifanya kwa malengo, na sio kuandika kama hobby/ilimradi—ni moja ya vitu ambavyo vinakula muda, vinachosha na vina vu-vitu vwingi vudogo vudogo ambavwo unabidi kuvushika na kuvufanya sehemu ya routine yako ya kila siku ili walau uweze kuandaa mambo yaliyotulia na yanaoonesha matokeo(ikiwa huna tools zozote za kukuraisishia workflow yako).


Utangulizi

Kwa kawaida, kama kipo kitu kinaweza kukuraishia mambo na kufanya kazi yako ya kuandaa, kuandika, na kupangilia makala zako kua nyepesi, basi it’s only logical that you get to use them.That said, ifuatayo ni orodha ya tools ishirini(10) nzuri na muhimu za kuwa nazo ili uweze kurahisisha kazi yako kama Blogger.

Unaweza kusoma pia: Namna Ya Kuandika Makala Zilizotulia Ili Uweze Kuwafikia Watu Wengi Zaidi

1. Grammarly

Kama umefungua blog ukiwa na malengo ya kuiunga Adsense na unaandika makala za Kingereza kwenye blog yako na ungependa ka kitu katakokua kanakusaidia kwenye kuhakikisha mambo unayoandika yako Grammatically Correct na Spelling ziko sawa, basi tool ya kuanza nayo ikiwa ya kwanza ni Grammarly.

Grammarly wako na Software unayoweza ku download kwenye laptop yako ambako unaweza kupaste makala yako nayo ita suggest sehemu gani ufanye marekebisho, iwe ni Spellings, Grammar, Semantic au kama uko na Syntax error.

Kama unaandikia kwenye Browser, wako na Extension unayoweza kuadd kwenye Google Chrome nayo itakua ina appear kila ukiwa unaandika na kusuggest marekebisho.

Pia wako na Keyboard, kwa ajili ya watumiaji wa simu na huduma zao zipo za bure na za kulipia pia. Japo for Basics, free plan inajitosheleza.

2. Google Docs

Moja ya Tools nyingine nzuri, za muhimu na bure kutumia ni Google Docs. Ambayo unaweza ipata na kuitumia kwa kudownload app kwenye simu yako, au kuiaccess directly kwenye Browser yako kwa kwenda ‘docs.google.com’

Google Docs inakupa option ya kuandika makala zako/iwe ni idea au Outline za post utakazo andika baadae.Na kama unashirikiana na mtu mwingine kuandika unaweza wapa access kwenye document husika nae akaandika na wewe.(Hii iko ideal kama unaandika, na una mtu mwingine ambae labda kazi yake ni kupitia makala zako na kurekebisha Spelling Errors, Semantics, nk)

3. Google Keyword Planner

Moja ya tools za mhimu zaidi ambazo kila Blogger ambaye yuko serious na kitu anafanya anabidi aiweke karibu ni Google Keyword Planner.Na hii utaitumia kufanya research, wakati unaandika makala zako kujua keyword gabi ni nzuri na zina traction hivyo uweze kufanya makala zako zifanye kazi vizuri SEO-Wise.

Kama hufahamu keyword ni nini, SEO, umuhimu wake nk, nitaandika makala hivi karibuni ambapo nitaelezea umuhimu wake kwa ufupi. Nayo utaweza kuikuta hapa ikishakua live.

4. Yoast SEO

Hapo hapo kwenye SEO, tool nyingine ya kuweka karibu ni Yoast SEO (kwa wale wenye Blog za WordPress)Ili uweze kuelewa umuhimu wake ni moaka uwe na uelewa kuhusu SEO, ni nini umuhimu wake, na kwanini blog yako inabidi iwe nayo.

Ingekua niileze kwa ufupi mno, SEO ni mjumuiko wa mambo ambayo unayafanya kuhakikisha blog yako inatokea kwete Search Engines kama Google, Bing, nk ili uweze kupata traffic ya kutosha.

Plugin hii ni bure, japo ipo na Premium version yake, na Addons nyingine kadhaa ambazo ni za kulipia. (Ikitokea nikakufanyia mimi SEO, basi Premium version nakuwekea bure).

Kama una Blog ya WordPress tayari, Yoast SEO plugin unaweza kuipata kwa kwenda kwenye Dashboard Yako, kisha Plugins»Add New kisha kusearch ‘Yoast SEO’

5. Pixellab

Pixellab ni app ya kwenye simu ambayo unaweza kuitumia kuunda Graphics ambazo ziko complicated au nyepesi, inategemea na mahitaji yako.Kwa kuanza inachanganya kidogo lakini ukiizoea unaweza itumia kuunda vu designs simple simple na hata vule vulivokaa Professional.

The upside ni kwamba ni ya bure ikiwa na features zote. Unalipia kama tu unataka kuondoa matangazo.

6. Unsplash

Picha ni element moja wapo muhimu kwenye uandishi wa Blog Posts, na sehemu unakoweza kupata picha ambazo ni Royalty Free (unazoweza kuzitumia hata katika namna zinazokuingizia pesa) huwa ni kipengele.Na hapa ndipo inapoingia Unsplash.

Ni tovuti unakoweza kuingia na kudownload picha za aina yoyote ile. Collection yao nzima iko Royalty free hivyo unaweza kuzitumia kwenye blog yako na hazina madhara yeyote ile kwako SEO-Wise au hata ukija kua na Adsense.Tovuti nyingine unazoweza tumia ni Pexels na Pixabay.

7. Google Search Console

Tool nyingine ya maana kutoka Google ni hii Google Search Console. Hii inakuruhusu ku verify umiliki wa domain yako, na kukupa access na ku control namna links za blog yako zitakavyokua zinaonekana kwenye Search Results.

Hivyo kama una blog na haiko connected na Google Search Console, fanya hivyo.

8. Forest App

Hii ni app ambayo unayoweka kwenye simu. Kazi yake ni kukufanya usishine simu .Unaweza kuipata kwa kwenda App Store/Playstore na kusearch ‘Forest App’

Ukishaiweka, unakua unaitumia muda ukiwa unataka kuandika makala zako na huitaji distractions zozote zile kutoka kwejye simu yako.

9. Google Keep Notes

Tool nyingine ya maana ambayo pia ni app ni hii Google Keep. Nayo ni app ya kutunza notes unayoweza itumia kuandika idea zako za blog posts.Kuweka To-Do Lists, Outlines, kuset Reminders na mengine mengi.

Feature pendwa kwa hii Note keeping app ni kwamba inatunza notes zako kwenye Cloud na iko connected na email yako.

Hivyo notes zako na mambo unayoandika hayawezi potea hata ukibadili simu. Na unaweza ya access kwa device yeyote ile yenye email yako.

10. Kainetics Blog

Haha kama matani vile. Sema niko serious kidogo. Kama ni blogger na uko serious na kitu unafanya; haijalishi ni Pro already au ni Beginner na unajifunza, basi ni muhimu kuwa na sehemu unako weza kurefer kujifunza kitu, na kuuliza maswali ukikwama kwa wengine ambao tayari wanafanya au wamefanys kile kitu ambacho unafanya.

Ziko sehemu nyingi ambako unaweza fanya ivo ila hii blog, ndiyo blog pekee ambako utaweza pata hizi madini kwa Kiswahili, kwa kina na kwa lugha simple inayoeleweka.Ukiwa na maswali/au ukawa na changamoto ambayo sijaandika kuihusu, unaweza nicheck WhatsApp.

Ukitaka kufanya kazi na mimi na ungependa kufahamu taratibu, au kujua ni vitu/huduma gani ninazo toa; unaweza kugusa hapa kusoma kuhusu Huduma Zangu kwa kina.

Hitimisho

That’s all. Hizo ndizo tools kumi za muhimu ambazo unabidi uwe nazo kuraisisha your whole process kama Blogger.Ni wewe kuangalia unahitaji ku archieve kitu gani na kuangalia ipi inaweza kufanikisha kitu unachotaka.Kwa maswali/maoni au kama kuna kitu cha kuongezea usisite ku comment.


Discover more from Kainetics

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Categorized in:

Blogging, Jifunze,